Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Simba kuikosa CECAFA

Muktasari:

  • Wambui alipata majeraha hayo wakati Simba Queens ikiwa nchini Kenya katika maandalizi ya mashindano hayo, jambo lililomlazimu kubaki nchini humo kwa ajili ya kuendelea na matibabu huku kikosi kikielekea Rwanda.

MSHAMBULIAJI wa Simba Queens, Elizabeth Wambui atakosa mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake yanayoendelea Rwanda baada ya  kuumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ulinzi Starlets.

Wambui alipata majeraha hayo wakati Simba Queens ikiwa nchini Kenya katika maandalizi ya mashindano hayo, jambo lililomlazimu kubaki nchini humo kwa ajili ya kuendelea na matibabu huku kikosi kikielekea Rwanda.

Kocha Mkuu wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’ alisema hadi sasa bado hawajapata majibu ya kina kuhusu tatizo linalomsumbua mshambuliaji huyo.

“Bado hatujafahamu tatizo lake vizuri hadi pale tutakapopata majibu kutoka kwa daktari. Lakini hatakuwepo kwenye mashindano haya,” alisema Mgosi.

“Ni pengo kwetu sisi ili kuweza kumfariji ni kufanya yeye alichokuwa anatamani kufanya na kuiona Simba queens ikiwa mabingwa wa cecafa hiyo ndio ahadi yetu kwake,”

Kukosekana kwa Wambui ni pigo kwa Simba Queens kutokana na nafasi yake katika kikosi hicho ambacho licha ya kuwa nyota mbalimbali kama Aisha Mnunka, Senaf Demise lakini ana uzoefu mkubwa.

Nahodha wa Simba, Ester Mayala, amesema timu hiyo itapambana kwa nguvu zote ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Wambui ambaye anatamani kuona Simba Queens ikitwaa ubingwa wa mashindano hayo.

Mayala ameongeza kuwa wachezaji wote wamebeba jukumu la kuhakikisha wanafanya vizuri na kumpa sababu ya kutabasamu Wambui wakati akiendelea na matibabu yake.

“Tunampa pole na ndio majukumu yetu. Amefanya kwa nafasi kubwa, tunaenda kuweka nguvu yote kwa sababu yako. Ninaamini tupo,” alisema nahodha huyo.

Simba imepangwa kundi C kwenye michuano ya CECAFA na Top Girls ya Burundi na Kenya Police ya Kenya.