Ugumu wa ratiba mechi tano za kwanza EPL
Muktasari:
- Msimu ulianza kwa mabingwa watetezi Arsenal kuwakaribisha mabingwa wa Championship msimu uliopita, Coventry City, kwenye Uwanja wa Emirates.
IPSWICH, ENGLAND: MSIMU wa Ligi Kuu England (EPL) 2026/27 ulianza jana Ijumaa, lakini ni klabu zipi zina ratiba ngumu zaidi mwanzoni mwa msimu, na zipi zina ratiba rahisi zaidi?
Msimu ulianza kwa mabingwa watetezi Arsenal kuwakaribisha mabingwa wa Championship msimu uliopita, Coventry City, kwenye Uwanja wa Emirates.
Huu ni msimu mwingine wa kusisimua katika vita ya juu ya kuwania ubingwa wa michuano hiyo na pia chini ya msimamo.
Lakini, bila shaka, kila timu itacheza mechi 38 katika msimu huo, huku ikikabiliana na wapinzani waliopo. Hata hivyo, mpangilio wa mechi hizo una umuhimu mkubwa. Kuanza msimu vizuri kunaweza kuamua mafanikio au kushindwa kutoboa ndani ya msimu mzima.
Ni timu moja pekee iliyowahi kutwaa ubingwa EPL baada ya kupoteza zaidi ya mechi moja katika mechi zake tano za mwanzo.
Ilikuwa Manchester United msimu wa kwanza wa Ligi Kuu England, 1992/93, ilipopoteza mechi mbili. Hata hivyo, wakati huo kulikuwa na mechi nne zaidi za kurekebisha hali hiyo kwa sababu ligi ilikuwa na timu 22.
Kwa timu zinazotarajiwa kuwa karibu na mkiani mwa msimamo, kuanza msimu kwa matumaini au kwa kukatisha tamaa kunaweza kuweka mwelekeo wa msimu wao. Kwa ujumla, timu 103 zimewahi kushinda mechi zao mbili za kwanza za msimu wa ligi hiyo, na ni tatu tu kati ya hizo zilizoshuka daraja katika msimu huo ambazo ni Wolves (2011/12), Hull City (2016/17) na West Bromwich Albion (2017/18).
Tottenham Hotspur ilikaribia kuwa timu ya nne msimu uliopita, lakini hatimaye ilipambana kuhakikisha inabaki Ligi Kuu England siku ya mwisho ya msimu.
Kwa hiyo, kufanya vizuri mwanzoni mwa msimu kunaweza kuleta tofauti kubwa. Hapa ndipo tathmini ya ugumu wa ratiba inaweza kutoa picha nzuri ya namna kila timu inavyoweza kufanya katika mwanzo wa msimu.
Kwa kuwa kutakuwa na mechi tano za Ligi Kuu England kabla ya mapumziko marefu ya wiki tatu ya mechi za kimataifa kuanza mwishoni mwa Septemba hivi ndivyo inavyoweza kuwa.
Ugumu wa ratiba katika mechi tano za kwanza, kwa mujibu wa Opta Power Rankings, ni mwanzo mzuri kiasi kwa Andoni Iraola katika kazi yake kama kocha wa Liverpool, ambapo mechi yake ya kwanza itampeleka St James Park kucheza dhidi ya Newcastle United katika mechi ya kwanza.
Huo siyo uwanja rahisi kucheza, lakini kwa kuwa kocha Eddie Howe pamoja na wachezaji muhimu Bruno Guimaraes, Anthony Gordon na Sandro Tonali wameondoka, huenda huu ukawa wakati mzuri wa kukutana na Newcastle United.
Baada ya hapo Liverpool itacheza dhidi ya Nottingham Forest nyumbani, Ipswich Town ugenini na Fulham nyumbani kabla ya kurejea Bournemouth katika mechi ya tano.
Wapinzani wa Liverpool katika mechi hizo tano wana wastani wa 91.2, ambao ni wa chini zaidi kati ya timu zote za Ligi Kuu katika mechi ya kwanza hadi ya tano.
Manchester City
Kumekuwa na mabadiliko mengi Manchester City msimu huu wa kiangazi, huku kocha Pep Guardiola akibadilishana na Enzo Maresca kwenye benchi la ufundi. Kiungo muhimu kikosini Rodri pia ameondoka na kujiunga na Barcelona, ingawa usajili wa Elliot Anderson kwa ada ya Pauni milioni 116 unaweza kusaidia kuziba pengo hilo.
Bahati nzuri kwa Maresca pia ana ratiba ambayo siyo ngumu sana katika mechi tano za kwanza, angalau kwa kuangalia kwenye karatasi. Hata hivyo, safari ya mechi ya nne kwenda kwa wapinzani wao wa jiji, Manchester United, inaweza kuwa ngumu iwapo City itaanza vibaya katika mechi zake tatu za kwanza.
Manchester United
Manchester United pia imepewa moja ya ratiba rahisi zaidi za mwanzo wa msimu. Cha kushangaza, kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2016/17, Red Devils wataanza msimu kwa kucheza ugenini. Hata hivyo, angalau watakutana na Hull City, timu iliyoorodheshwa kuwa ya mwisho kwa ubora katika ligi.
Baada ya hapo, kikosi cha Michael Carrick kitawakaribisha Ipswich Town, timu nyingine iliyopanda daraja kabla ya kusafiri kwenda kucheza na Everton.
Carrick atataka kuendeleza kasi nzuri ambayo United ilimalizia nayo msimu wa 2025/26 chini ya uongozi wake, na sasa akiwa amepewa kazi hiyo akiwa kocha wa kudumu Old Trafford.
United ilikusanya pointi 39, ambazo zilikuwa nyingi kuliko timu nyingine yoyote, tangu Carrick alipoteuliwa Januari 2026. Hiyo ilikuwa pointi tatu zaidi ya Arsenal.
Arsenal
Arsenal inaanza msimu ikiwa bingwa mtetezi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 22, hivyo presha itakuwa kubwa kwao kufanya vizuri tangu mwanzo.
Mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya Coventry City, timu iliyopanda daraja, imepewa kiwango cha moja ya ratiba nzuri zaidi za kuanzia msimu wa Ligi Kuu England. Hata hivyo, baada ya hapo Arsenal itaifuta Aston Villa kabla ya kukutana na Chelsea katika Dabi ya London kwenye Uwanja wa Emirates. Hivyo, mechi ya pili na tatu zitakuwa na mitihani migumu zaidi.
Coventry City
Frank Lampard aliiongoza Coventry kutwaa ubingwa wa Ligi ya Championship msimu uliopita, huku ikimaliza ikiwa na tofauti ya pointi 11 dhidi ya Ipswich. Lakini, zawadi yao kwa mafanikio hayo ni kupewa ratiba ngumu zaidi ya mwanzo wa msimu.
Wapinzani watano wa kwanza wa Sky Blues wana wastani wa alama nzuri wanazopewa na Opta kuondoka na ushindi. Sehemu kubwa ya ugumu huo inatokana na mechi zao za ugenini dhidi ya timu mbili zilizomaliza juu msimu uliopita ambazo ni Arsenal na Manchester City.
Bournemouth
Bournemouth ina ratiba ngumu zaidi kwa pamoja na Coventry, huku kocha mpya Marco Rose akikabiliwa na mwanzo mgumu wa kazi yake.
Mechi ya kwanza itakuwa safari ya kutisha kwenda Etihad Stadium kukutana na Manchester City katika mechi ya kwanza.
Bournemouth pia itaingia katika mapumziko marefu ya mechi za kimataifa baada ya kuikaribisha klabu yake ya zamani, Iraola, kwenye Uwanja wa Vitality, Jumapili, Septemba 20.
Sunderland
Itakuwa jambo la kuvutia kuona Sunderland itakabilianaje na ratiba kutokana na kushiriki mashindano ya klabu ya Ulaya msimu huu, baada ya kumaliza katika nafasi ya saba msimu uliopita.
Kikosi cha Regis Le Bris kitacheza angalau mechi nane za ziada kutokana na kufuzu UEFA Europa League, na hilo pia litailazimisha kucheza ratiba ngumu ya Alhamisi hadi Jumapili, au Alhamisi hadi Jumatatu, katika sehemu ya kwanza ya msimu wa 2026/27.
Mechi tano za kwanza za Sunderland katika Ligi Kuu England zimepewa kiwango cha ratiba ya tatu kwa ugumu zaidi kati ya timu 20. Sababu kubwa ni mechi ya nne na tano dhidi ya Arsenal na Manchester City.