Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Namungo aandika rekodi tatu

NAMUNGO Pict

Muktasari:

  • Matiko  anakumbukwa zaidi kwa kuibuka Mfungaji Bora wa Michuano ya Majeshi ya CDF Cup 2026, baada ya mshambuliaji huyo kufunga mabao 10.

MSHAMBULIAJI wa Namungo FC, Gamba Iddi Matiko ameandika rekodi tatu akiwa na kikosi hicho baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Coastal Union, ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Oktoba 24, 2025 kwenye Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.

Katika mechi hiyo, Matiko alifunga bao moja dakika ya kwanza na lingine likifungwa na Herbert Lukindo dakika ya 67, huku la Coastal Union likifungwa na Shiza Kichuya dakika ya tisa.

Baada ya bao hilo la Matiko, nyota huyo ameandika rekodi tatu, ya kwanza ni ya kufunga bao la mapema zaidi msimu huu Ligi Kuu Bara, ya pili ni la kwanza kwake akiwa na Namungo tangu ajiunge na kikosi hicho msimu huu na tatu ni ya kuvunja rekodi ya Bakari Msimu.

NAMU 01

Tangu msimu huu wa 2026-2027 umeanza, bao hilo ndilo la mapema zaidi kufungwa katika Ligi Kuu Bara likichukua sekunde 17, baada ya kumalizia kwa kichwa krosi iliyopigwa na Rashid Chambo.

Bao hilo limemfanya Matiko kuvunja rekodi ya msimu uliopita iliyokuwa inashikiliwa na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Coastal Union, Bakari Msimu aliyefunga sekunde ya 58, wakati timu hiyo ilipoichapa Tanzania Prisons mabao 4-1.

NAMU 02

Matiko  anakumbukwa zaidi kwa kuibuka Mfungaji Bora wa Michuano ya Majeshi ya CDF Cup 2026, baada ya mshambuliaji huyo kufunga mabao 10.