Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki IAA SC avunja ukimya

MGANGA Pict

Muktasari:

  • Beki huyo aliyewahi pia kuichezea Mbeya Kwanza, Ruvu Shooting, Namungo FC, Pamba Jiji, Ndanda FC, Tabora United kwa sasa TRA United, KenGold FC na Mbeya City, amesema ubora wa mabeki wenzake unampa motisha ya kupambana bila ya kukata tamaa.

BEKI wa kati wa IAA SC ya jijini, Arusha, Faisal Richard Mganga amesema licha ya kutopata nafasi ya kucheza hadi sasa katika timu hiyo, ila ataendelea kupambana kwenye uwanja wa mazoezi, ili kushawishi benchi la ufundi kumtumia kikosini.

Faisal amesema tangu ajiunge na timu hiyo mambo yamekuwa magumu kwa sababu hajapata nafasi ya kucheza hata mechi moja, tofauti na ilivyokuwa akiwa KenGold ya jijini Mbeya, aliyoachana nayo baada ya mkataba kuisha.

“Wakati naichezea KenGold nilikuwa napata nafasi ya kucheza mara kwa mara ila kwa hapa IAA SC imekuwa tofauti, ushindani ni mkubwa na kila mchezaji anapambana kumshawishi kocha kumtumia, kwangu ni changamoto ninayopambana nayo pia,” amesema.

Beki huyo aliyewahi pia kuichezea Mbeya Kwanza, Ruvu Shooting, Namungo FC, Pamba Jiji, Ndanda FC, Tabora United kwa sasa TRA United, KenGold FC na Mbeya City, amesema ubora wa mabeki wenzake unampa motisha ya kupambana bila ya kukata tamaa.

“Nafasi moja inapokuwa na zaidi ya wachezaji wawili hadi watatu wazuri maana yake ushindani lazima uwe mkubwa kwa kila mmoja kutaka kucheza, binafsi napenda ushindani kwa sababu unanifanya nipambane wakati wote mazoezini,” amesema Faisal.