Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stam bado hakijaeleweka TMA FC

STAM Pict

Muktasari:

  • Stam amejiunga na TMA FC akichukua nafasi ya Haji Ali Nuhu ambaye kwa sasa ni Kocha Msaidizi wa Namungo FC chini ya Juma Mgunda na katika mechi zake tano, imeshinda moja, sare moja na kupoteza tatu, ikishika nafasi ya 13 na pointi nne.

KOCHA Mkuu wa TMA FC, Amri Said 'Stam' amesema kwa sasa bado hajafikia uamuzi wa mwisho wa kuifundisha timu hiyo moja kwa moja, ingawa bado anaendelea kuisimamia kutokana na ushirikiano wake na viongozi wa kikosi hicho cha mjini, Iringa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Stam amesema licha ya kukifundisha kikosi hicho, ila bado hajasaini mkataba wowote hadi sasa, jambo ambalo linampa nafasi ya kufanya majukumu mengine pia nje ya timu hiyo, kwa sababu sio mwajiriwa wa moja kwa moja.

"Ninachofanya kwa sasa ni sawa na kujitolea kutokana na ushirikiano wangu mzuri na watu wa Iringa, TMA FC ni timu nzuri sana kwa sababu ina wachezaji vijana na wenye kiu ya mafanikio, ingawa, bado inahitaji kupewa muda zaidi," amesema Stam.

Kocha huyo aliyewahi kuzifundisha Simba, Fountain Gate, Bigman FC zamani Mwadui FC, Lipuli FC, Mbao FC, Biashara United, Mbeya City na KVZ FC ya visiwani Zanzibar, amesema mwenendo wa timu hiyo sio mzuri, ingawa kuna matumaini zaidi mbeleni.

Stam amejiunga na TMA FC akichukua nafasi ya Haji Ali Nuhu ambaye kwa sasa ni Kocha Msaidizi wa Namungo FC chini ya Juma Mgunda na katika mechi zake tano, imeshinda moja, sare moja na kupoteza tatu, ikishika nafasi ya 13 na pointi nne.