Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Championship ni kicheko na vilio

Muktasari:

  • Hadi sasa ligi hiyo imefikia mzunguko wa tano, huku ikisubiriwa raundi ya sita itakayopigwa wikiendi hii ikishuhudiwa wababe Stand United kuwafuata Bandari Tanzania, Transit Camp kuwakaribisha KMC, Mtibwa Sugar dhidi ya Tanzania Prisons na IAA dhidi ya Rhino Rangers

WAKATI timu nne zikihaha kusaka ushindi wa kwanza Championship, nyingine mbili zimeonekana kuwa na rekodi ya kipekee zikicheza mechi tano bila kupoteza na kujiweka katika nafasi nzuri kuwania kupanda Ligi Kuu.

Hadi sasa ligi hiyo imefikia mzunguko wa tano, huku ikisubiriwa raundi ya sita itakayopigwa wikiendi hii ikishuhudiwa wababe Stand United kuwafuata Bandari Tanzania, Transit Camp kuwakaribisha KMC, Mtibwa Sugar dhidi ya Tanzania Prisons na IAA dhidi ya Rhino Rangers.

Katika mechi zilizopigwa hadi sasa, timu nane hazijaonja ushindi ikiwa ni Gunners iliyoambulia sare tatu na kupoteza mechi mbili sawa na Songea United, huku TMA na Bigman zikitoa sare moja na kupoteza minne.

Transit Camp inayoongoza ligi kwa pointi 13 na KMC pointi 11 hazijapoteza mchezo wowote na kujiweka kwenye mwelekeo mzuri wa kupanda Ligi Kuu, huku  Tanzania Prisons yenye pointi 10 nafasi ya tatu na Kigamboni United zikipoteza mmoja.

Kocha Mkuu wa Prisons, Shedrack Nsajigwa alisema matokeo waliyonayo si mabaya wala mazuri sana, badala yake wachezaji ni kuendelea kupigania nembo ya timu hiyo kurejea Ligi Kuu.

“Ligi ni ngumu kila timu inaonesha kujipanga kufikia malengo, hatujawa na matokeo mazuri au mabaya sana japokuwa tulihitaji kuwa kileleni, lazima tujipange zaidi kwa mechi zinazofuata,” alisema Nsajigwa.

Kocha Mkuu wa KMC, Mohamed Muya alisema kiu yao ni kuona wanarejea tena Ligi Kuu akieleza kuwa kila mechi kwao ni vita ya pointi tatu, akikiri kuwapo ushindani na ugumu wa michuano hiyo.

“Hatujaanza vibaya lakini tunahitaji kupambana zaidi bado ni mapema na yeyote anaweza kufanya lolote wakati wowote, championship ni ligi ngumu kwakuwa kila kitu inapambana,” alisema kocha huyo.