Simba yapigwa 'stop' kusajili

Muktasari:

  • Taarifa mbaya kwa mashabiki wa Simba ni kwamba Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeifungia klabu hiyo kusajili kwa kipindi kimoja kijacho cha usajili.

Taarifa mbaya kwa mashabiki wa Simba ni kwamba Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeifungia klabu hiyo kusajili kwa kipindi kimoja kijacho cha usajili.
Nyundo hiyo ya FIFA imekuja kufuatia shirikisho hilo kuikuta na hatia Simba kutokana na kushindwa kumalizana na beki wao wa zamani, Mghana Asante Kwasi.

Taarifa kutoka nchini Ghana zinasema adhabu hiyo kwa Simba itaanza kufanya kazi katika dirisha lijalo la usajili.

Taarifa kamili kuhusu adhabu hii endelea kufuatilia Mwanaspoti.