Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaendelea kuikaba Yanga, Geita ikiendeleza unyonge

SIMBA Pict

Muktasari:

  • Yanga iliyocheza mapema leo saa 10:00 jioni, iliifunga Fountain Gate mabao 2-0 na kufikisha pointi 15, baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara kushinda mechi tano mfululizo.

USHINDI wa Simba wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold, umekifanya kikosi hicho kuendelea kuikaba Yanga katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, huku timu hizo zikitofautiana mabao baada ya zote kushinda mechi zao tano mfululizo na kukusanya pointi 15.

Yanga iliyocheza mapema leo saa 10:00 jioni, iliifunga Fountain Gate mabao 2-0 na kufikisha pointi 15, baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara kushinda mechi tano mfululizo.

Kwa upande wa Simba ikicheza kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es Salaam, ilianza kutikisa nyavu za wapinzani dakika ya 21, kupitia kwa Mzambia, Clatous Chama aliyemalizia vyema pasi ya Libasse Gueye anayefikisha asisti tano.

Bao hilo la Chama ambalo ni la tatu kwake msimu huu katika Ligi Kuu, liliifanya Simba kuendelea kutengeneza mashambulizi, huku Geita Gold ikicheza kwa tahadhari ya kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza na mechi hiyo kwenda hadi mapumziko kwa kikosi hicho cha Msimbazi kuongoza dakika 45 za kwanza.

SIMB 02

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, japo Simba ilipata bao la pili dakika ya 59, lililofungwa na Libasse Gueye aliyetumia vyema pasi ya Nathaniel Chilambo na kukihakikishia kikosi hicho pointi tatu.

Ushindi huo unaifanya Simba kushinda mechi tano mfululizo za Ligi Kuu Bara msimu huu ikiwa na pointi 15, ambazo ni sawa na watani zao wa jadi Yanga inayoongoza kwa tofauti ya mabao.

Kwa upande wa Geita Gold iliyorejea Ligi Kuu msimu huu, kichapo cha leo ni cha pili msimu huu katika Ligi Kuu Bara, baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC, Agosti 18, 2026.

Katika mechi tano ilizocheza Geita Gold msimu huu, imeshinda mbili, ikipoteza mbili na sare moja kati ya tano, huku ikishika nafasi ya sita na pointi saba kwenye msimamo.

SIMB 01

Ushindi huu kwa Simba umeifanya timu hiyo kuendeleza rekodi nzuri dhidi ya Geita Gold, kwani mara ya mwisho kukutana kabla ya leo ilishinda mabao 4-1, mechi iliyopigwa, Mei 21, 2024.

Katika mechi hiyo ya Mei 21, 2024, mabao ya Simba yalifungwa na Mrundi Saidi Ntibazonkiza 'Saido' na Ladack Chasambi waliofunga mawili kila mmoja wao, huku bao pekee la Geita Gold likifungwa na Geofrey Julius.

Aidha, Geita Gold imeendeleza rekodi mbovu kwani tangu ilipoanza kucheza Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza msimu wa 2021-2022, haijawahi kushinda dhidi ya Simba, baada ya kuchapwa mechi sita na kutoka sare moja tu kati ya saba walizokutana.