Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba v Mighty Wanderers utamu wa mechi upo hapa!


BAADA ya msimu uliopita kuwa na matokeo mabaya kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba leo inaanza tena kazi ya kuhakikisha inafuta jinamizi baya watakapowakabiri Mighty Wanderers ya Malawi, kwenye mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa.


Kwa mashabiki wa soka, leo ni siku ya kushikilia rimoto mkononi kwa dakika tisini ili kuhakikisha wanaangalia kila kitu kuhusu mchezo huo.

Msimu uliopita, Simba ilishika mkia katika hatua ya makundi, anguko ambalo haikuwahi kulipata mara zote ilizowahi kuingia hatua hiyo huko nyuma hivyo hapana shaka inaingia msimu huu ikiwa na lengo la kurudi katika njia yake kwenye mashindano hayo.

Hata hivyo, ili hilo litimie, ni lazima Simba ipenye mbele ya Mighty Wanderers, jambo linalochangia kuifanya mechi ya leo ugenini ambayo ni ya raundi ya kwanza ya awali iliyopangwa kuchezwa katika Uwanja wa Taifa wa Bingu, uliopo Lilongwe, Malawi kuwa muhimu kwa wawakilishi hao wa Tanzania, wakihitajika kupata ushindi ambao utawaweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Ukiachana na uzoefu wa mashindano ya kimataifa ambao Simba wamekuwa nao, wawakilishi hao wa nchi wanaingia uwanjani katika mchezo huo uliopangwa kuanza saa 10:00 kwa muda wa Tanzania wakiwa muendelezo bora wa kiwango na matokeo mazuri katika mechi walizocheza hivi karibuni.

Simba inakabiliana na Mighty Wanderers leo ikiwa imetoka kupata ushindi katika mechi zote tano ilizocheza za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ambapo imefunga mabao tisa na imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara mbili tu.

Wenyeji wao Mighty Wanderers, katika mechi tano zilizopita hivi karibuni ambazo zote ni za Ligi Kuu ya Malawi, wamepata ushindi mara tatu huku wakifunga mabao saba na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara tatu.

Winga Libasse Gueye anaingia kwenye mchezo wa leo kama mchezaji anayetegewa zaidi na Simba kutokana na kiwango bora ambacho anaendelea kukionyesha katika timu hiyo hasa katika kuzalisha mabao.

Kati ya mabao tisa ambayo Simba imeyafunga kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, winga huyo wa Senegal pekee amehusika na mabao sita akifunga moja na kupiga pasi tano za mwisho.

Historia tamu kwa Simba katika ardhi ya Malawi na Uwanja wa Bingu ni kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya raundi kama hii, Septemba 2022, ilipoichapa Nyasa Big Bullets ya huko.

Kocha wa Simba, Steve Barker amesema kuwa kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wa leo.

“Bila shaka wao (Mighty Wanderers) ni timu nzuri. Wanashindania tena ubingwa wao wa Ligu Kuu Malawi. Tumekuja hapa kutafuta matokeo mazuri na sio vinginevyo. Tunataka kuhakikisha kile ambacho tumekifanya kwenye ligi kinaonekana pia kwenye mechi za kimataifa,” alisema Barker.


SINGIDA BS NAYO WAMO

Katika Kombe la Shirikisho Afrika, wawakilishi wengine wa Tanzania, Singida Black Stars watakuwa na kibarua cha ugenini dhidi ya Al Ghazala katika mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Juba nchini Sudan Kusini.

Mchezo huo umepangwa kuanzia saa 10:30 jioni.

Singida Black Stars inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kufika hatua ya makundi msimu uliopita.