Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba Queens yaahidi makubwa Kimataifa

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Simba Queens wanatarajiwa kuondoka nchini kesho Julai 14 kueleka Kenya kwa ajili ya michuao ya kushiriki Ligi ya Mabingwa ya Wanawake kanda ya Baraza la vyama vya Soka la Afrika Mashariki na kati (CECAFA).

Mashindano hayo ambayo yataanza kutimua vumbi Julai 17 Jijini Nairobi, Kenya.

Akizugumza Kocha Mkuu wa Kikosi hicho Mussa Hassan Mgosi alisema kuwa maandalizi ya safari yamekamilika na wanatarajia kuondoka nchini kesho Jumatano kulingana na majibu ya vipimo vya Covid-19 kukamilika na hii ni baada ya kumaliza kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya wanawake ya Twiga Stars (Jana).

"Mipango yetu ni kuelekea kenya mapema sana ili kuweza kuzoea hali ya hewa kwa sababu tumesikia hali ya kule ni baridi sana, hivyo mipango yetu ni kuondoka kesho baada ya kucheza mechi yetu ya kirafiki dhidi ya Twiga Stars na kama vipimo nya COVID-19 vikiwahi kufika mapema tunaweza kuondoka Jumatano (leo)" alisema Mgosi

Aidha Mgosi alisema kuwa wamejiandaa vizuri na ndio maana wameamua kuomba mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania 'Twiga Stars' kwa lengo la kujiweka fiti kabla ya kuanza michuano hiyo mikubwa na tayari wamewaona na kupata taarifa za wapinzani wao ambao wako nao kundi moja.

"Tunatarajia kwenda kufanya vizuri na kuhakikisha tunakuwa ni miongoni mwa timu ambazo zitakwenda nchini Misri, nina imani kubwa kuwa vijana wetu waliopo na hawa wapya watafanya vizuri kwa kutwaa ubingwa wa Cecafa na kuweza kupata tiketi ya kwenda kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ya Wanawake kwa kuwa hiyo ndiyo dhamira yetu kubwa,” alisema.

Simba Queens ambao waliingia kambini tangu Juni 17 wamekuwa wakifanya mazoezi ili kujiweka tayari kwa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Cecafa huku wakiwa wamefanya usajili kadhaa wa wachezaji kwa ajili ya kuboresha na kukiongozea nguvu kikosi hicho.

wachezaji waliosajiliwa ni pamoja na beki wa kati Wema Richard Maile aliyetokea Mlandizi Queens, kiungo wa kati Danai Bhobho aliyetokea Harare City Queens ya Zimbabwe na Mshambuliaji Aisha Juma Mnunka kutoka Alliance Girls.

katika michuano hiyo Simba wamepangwa kwenye Kundi (A) pamoja na timu ya PVP FC ya Burundi na Mabingwa wa Uganda Lady Doves WFC.

Kundi (B) linaundwa na timu ya Bank ya Biashara ya Ethiopia (CBE), Yel Joint Stars ya Sudan Kusini na New Generation Queens ya Zanzibar huku Scandinavia WFC ya Rwanda, (FAD) ya Djibout na Vitiga Queens ya Kenya zikiwa kwenye kundi C.

Mshindi wa jumla kutoka kwenye kila makundi matatu ya kanda ya CECAFA ndio ataenda nchini Misri kushiriki Ligi  ya Mabingwa Afrika ya Wanawake ambayo itafanyika mapema mwaka huu ikihusisha Mabingwa wa kanda nyingine za Afrika.


IMEANDIKWA NA DAUDI ELIBAHATI