Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba kuangukia kwa wababe hawa...

Baada ya kufuzu hatua ya makundi Klabu ya Simba inasubiri droo itakayopangwa Januari 8, 2021 kujua wapinzania wao.

Simba imefika hatua hiyo baada ya kushinda mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe licha ya kufungwa bao 1-0 kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa Zimbabwe.

VIDEO: Simba kuangukia kwa wababe hawa...

Simba ilipata bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa na Erasto Nyoni, bao la pili limefungwa na Shomari kapombe akimalizia mpira uliotemwa na kipa Francis Tizayi, bao la tatu likiwekwa na John Bocco akimalizia mpira laini aliotengewa na Bwalya huku Clatous Chama akimaliza bao la nne kwa mkwaju wa penalti baada ya kuchezwa madhambi.

Timu zote zimetengwa kwenye makundi (pot) nne kutokana na pointi walizonazo na Simba ipo pot 3 na timu za Petro de Luanda ya Angola na MC Alger ya Algeria.

Katika pot hiyo Simba watasubiri timu moja baada ya kutochezwa kwa mechi ya marudiano ya Al Hilal ya Sudan dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana baada ya Kotoko kugoma kucheza kwa madai mchezaji wao mmoja hajapatiwaa majibu yake ya vipimo vya corona.

Kwa mantiki hiyo Simba atasubiri timu za pot 1, 2 na 4 ambazo zipo hivi;

Pot 1 - Al Ahly (Misri), Wydad Casablanca (Morocco), Esperance (Tunisia), TP Mazembe (Congo)

Pot 2- Zamalek (Misri), Mamelod Sundown (Afrika Kusini), Horoya (Guinea), AS Vita (Congo)

Pot 4- Al Merrikh (Sudan), CR Belouizdad (Algeria), Teungueth (Senegal), Kaizer Chiefs (Afrika Kusini)