Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siku ya wanawake Simba 1, Yanga 1

KAMA hujui ni kwamba, leo ni Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka tangu ilipoanza kuadhamishwa mwaka 1975 baada ya Umoja wa Mataifa (UNO) kuridhia ina maajabu makubwa kwa klabu za Simba na Yanga. Usibishe!

Kwa mashabiki wa Simba na Yanga, ni ngumu kuisahau, kwani ni mara mbili tu timu zao zimekutana ndani ya siku kama ya leo katika mechi za Ligi Kuu Bara na kila upande kutoka na ushindi mmoja na kupoteza mmoja.

Cha kushangaza mechi hizo mbili zina maajabu yanayofanana kiasi cha kushangaza na kuifanya Siku ya Wanawake iwe ya kipekee kwa timu hizo, hata kama baadhi ya mashabiki wameshasahau.

Ipo hivi. Timu hizo zilikutana kwa mara ya kwanza Machi 8, 2015 na Simba kushinda bao 1-0 ikiwa ni baada ya msoto wa kucheza mechi tano mfululizo mbele ya watani wao bila kupata ushindi tangu ilipoifunga Yanga kwa mabao 5-0 katika mechi iliyopigwa Mei 6, 2012.

Shujaa wa Simba katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam alikuwa ni Emmanuel Okwi aliyefunga bao hilo la pekee kwa shuti kali katika kipindi cha pili.

Okwi alifunga bao hilo dakika ya 52 baada ya kupokea pasi ya Ibrahim Ajibu kisha kumchungulia kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ na kumuona ametoka langoni na kupiga mashine iliyoenda moja kwa moja wavuni na kuipa Simba ushindi huo muhimu licha ya Yanga kupambana kutaka kulirudisha bao hilo.

Cha kuvutia ilikaa miaka mitano kabla ya Yanga nayo kujibu mapigo katika siku nyingine kama ya leo ya Machi 8, lakini ikiwa ni mwaka 2020 ilipoizamisha Simba pia kwa bao 1-0 katika mchezo mkali uliopigwa pia Jumapili.

Kali zaidi ni kwamba ambapo kama ilivyokuwa kwa Simba, nao Vijana wa Jangwani walijikomboa kwenye unyonge baada ya kumecheza mechi saba mfululizo za Ligi dhidi ya Wekundu bila kushinda tangu iliposhinda mara ya mwisho Febuari 20, 2016 kwa mabao 2-0.

Mkombozi wa Yanga katika pambano hilo lililopigwa pia Kwa Mkapa, alikuwa ni Benard Morrison aliyefunga kwa mpira wa friikikii dakika ya 44 baada ya Jonas Mkude kumchezea winga huyo Mghana madhambi nje ya 18 na BM33 akamchungulia kipa Aishi Manula na kuweka mpira kambani.

Rekodi zinaonyesha katika mechi hizo zilizopigwa Siku ya Wanawake Duniani, Simba ilishinda mechi mwaka 2015 ikiwa wenyeji na bao lake lililofungwa na nyota wa kigeni aliyekuwa msumbufu aliyewahi kukipiga timu hizo mbili, Emmanuel Okwi kutoka Uganda.

Kadhalika bao lililoikomboa Yanga mwaka 2020 ikiwa ndio wenyeji wa mchezo, lilifungwa pia na winga mtukutu aliyekipiga timu zote, Okwi.