Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Depu apishana na Komara Yanga 

Muktasari:

  • Depu alitua Yanga Januari 2026 na kupewa mkataba wa miaka miwili, akitokea Radomiak Radom ya Poland. Amecheza kwa takribani miezi sita na kuweka alama nzuri katika ufungaji akipachika mabao tisa ya Ligi Kuu Bara 2025-2026.

Yanga imefikia uamuzi kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wake, Laurindo Aurelio 'Depu', baada ya kupokea ofa nzuri kutoka Petro de Luanda inayotaka kumsajili katika dirisha hili kuelekea msimu wa 2026-2027.

Depu alitua Yanga Januari 2026 na kupewa mkataba wa miaka miwili, akitokea Radomiak Radom ya Poland. Amecheza kwa takribani miezi sita na kuweka alama nzuri katika ufungaji akipachika mabao tisa ya Ligi Kuu Bara 2025-2026.

Mwanaspoti linafahamu kuwa, viongozi wa Yanga wamefanyia kazi ofa hiyo na wamekubaliana kumruhusu nyota huyo kuondoka baada ya mazungumzo kukamilika.

Wakati huohuo, mabingwa hao mara tano mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, tayari wameziba nafasi inayoachwa na Depu kwa kumsajili beki wa kimataifa wa Ivory Coast, Oumar Farouk Komara, kutoka Golden Arrows ya Afrika Kusini.

Taarifa zinasema kocha Manqoba Mngqithi amehusika moja kwa moja katika kumpendekeza Komara kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja, jambo ambalo linaonekana kuwa muhimu katika mipango ya kiufundi ya timu hiyo kuelekea msimu mpya.

Chanzo kimesema ujio wa Komara una faida kubwa kwa Yanga, hasa katika kipindi ambacho beki wa kati, Dickson Job, bado hajarejea rasmi uwanjani baada ya kusumbuliwa na majeraha tangu msimu uliopita.

"Komara ni chaguo la benchi la ufundi. Ana uwezo wa kucheza beki na pia kiungo mkabaji, hivyo atatoa suluhisho kwenye maeneo mawili muhimu ndani ya kikosi," kimesema chanzo hicho.

Mbali na kucheza kama beki, Komara pia ana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji, jambo litakalompa kocha Manqoba chaguo zaidi katika kupanga kikosi kulingana na mahitaji ya kila mechi.

Usajili wa Komara na kuondoka kwa Depu, unafanya Yanga kuwa na idadi ya wachezaji 12 wa kigeni wanaotakiwa kikanuni ambao ni Komara, Fred Ngoma, Cheikh Ibrahima Touré, Albert Kangwanda, Housseine Zakouani, Peter Shalulile, Djigui Diarra, Kouassi Attohoula Yao, Chadrack Boka, Duke Abuya, Maxi Mpia Nzengeli na Allan Okello.