Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shindika apendekeza nafasi mbili za kuimarisha Tabora United

SHINDIKA Pict

Muktasari:

  • Katika maisha yake ya soka, Shindika aliwahi kuzichezea Simba, Mtibwa Sugar, Taifa Stars na Kongsvinger IL ya Norway. Akiwa mchezaji, alicheza zaidi nafasi ya kiungo mkabaji, lakini pia aliwahi kutumika kama beki wa kati.

KOCHA msaidizi wa Tabora United, Henry Joseph Shindika, amesema timu hiyo inahitaji kuongeza wachezaji wawili katika dirisha dogo la usajili la Januari 2027, akitaja nafasi ya beki wa kushoto na mshambuliaji kuwa maeneo yanayohitaji kuimarishwa zaidi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Shindika amesema kwa ujumla kikosi hicho hakina changamoto kubwa katika maeneo mengine, lakini kuongeza wachezaji katika nafasi hizo mbili kutasaidia kuleta uwiano na kuongeza ushindani ndani ya timu.

“Maeneo yote hayana shida sana, ila beki wa kushoto na mshambuliaji ndiyo yanayohitaji kufanyiwa maboresho zaidi. Dirisha dogo la Januari 2027 litakapofunguliwa rasmi, tayari tumeanza mchakato mapema na umefikia sehemu nzuri,” amesema.

Shindika, ambaye alijiunga na Tabora United baada ya kuachana na Fountain Gate aliyokuwa akihudumu kama kocha wa viungo na utimamu wa mwili, amesema maboresho hayo yanatarajiwa kuongeza ushindani ndani ya kikosi.

Katika maisha yake ya soka, Shindika aliwahi kuzichezea Simba, Mtibwa Sugar, Taifa Stars na Kongsvinger IL ya Norway. Akiwa mchezaji, alicheza zaidi nafasi ya kiungo mkabaji, lakini pia aliwahi kutumika kama beki wa kati.

Pia aliwahi kuhudumu Mtibwa Sugar katika majukumu mbalimbali, ikiwamo kuwa meneja wa timu za vijana chini ya miaka 20 na baadaye timu ya wakubwa.