Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shimmuta kuanza mwezi ujao Morogoro

SHIMUTA Pict

Muktasari:

  • Zaidi ya michezo 15 inatarijiwa kuchezwa baadhi ikiwa ni kurusha tufe, kurusha mkuki, michezo ya jadi, drafti, karata, pool table, kuruka kamba, soka, netiboli na riadha maalumu kwa wazee kuanzia miaka 50 ambapo watakimbia mita 800.

MASHINDANO ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Kampuni Binafsi Tanzania (Shimmuta) yanaanza Novemba 6 hadi 21,2026, Morogoro ambapo zaidi ya mashirika 100 yatashiriki.

Zaidi ya michezo 15 inatarijiwa kuchezwa baadhi ikiwa ni kurusha tufe, kurusha mkuki, michezo ya jadi, drafti, karata, pool table, kuruka kamba, soka, netiboli na riadha maalumu kwa wazee kuanzia miaka 50 ambapo watakimbia mita 800.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Masoko wa Shimmuta, Nicholous Ngowi amesema maandalizi yanaendelea vizuri ambapo dirisha la usajili lilifunguliwa na washiriki watajisajili kwa mfumo wa kidijitali wa shirikisho hilo.

Ngowi amesema timu zitakazoshiriki ni zile zitakidhi vigezo baada ya usajili wa wachezaji ambao utakuwa unafanywa na mkuu wa kila idara ya rasilimali watu wa shirika na baadaye kuidhinishwa na Shimmuta kwa alama za vidole.

“Kila timu shiriki kwanza inapaswa kulipa ada ya uanachama inayolipwa kila mwaka, ada ya ushiriki wa mashindano kwa kila timu, hizo pesa ndizo zinazotumika kwenye maandalizi na mambo mengine kama kulipia uwanja, matangazo, malazi, medali na kulipa waamuzi,” amesema.