Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkurugenzi TPA aanika siri kutwaa makombe Shimuta

Katibu wa Michezo TPA, Edna Kitila akimkabidhi kombe la mshindi wa jumla wa michuano ya Shimuta Mkurugenzi Mkuu, Erick Hamissi

Muktasari:

‘TUNAPAKIA tunapakua kazi kazi' hiyo ni kauli mbiu ya wachezaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakati wakimkabidhi makombe Mkurugenzi Mkuu, Erick Hamissi waliyoyatwaa hivi karibuni.

‘TUNAPAKIA tunapakua kazi kazi' hiyo ni kauli mbiu ya wachezaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakati wakimkabidhi makombe Mkurugenzi Mkuu, Erick Hamissi waliyoyatwaa hivi karibuni.

Wachezaji hao wa TPA walijinyakulia makombe matano katika michuano ya Shimuta yaliyofanyika Mkoani Morogoro mwezi uliopita.

Akizungumza na wanahabari Hamissi amesema, ushindi huo hawajabahatisha bali umetokana na umoja, mshikamano ambao wanao wafanyakazi wake.

Amesema alipoingia TPA Aprili 9 mwaka huu aliagizwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anaondoa makundi ambayo yalikuwepo, akikiri ni jambo ambalo amelifanikisha kwa asilimia kubwa na ndio maana wameweza kufanya vizuri.

"Nimefurahi kwa namna ambavyo mmeiwakilisha vizuri TPA katika mashindano hayo muhimu nawaomba awamu nyingine muendelee hivyo hivyo"

"Kama kauli mbiu yetu inavyosema tunapakua tunapakia kazi kazi, basi nawaomba umoja huu uendelee hata katika majukumu yenu ya kawaida, "

Amesema kitendo cha timu ya TPA kuibuka mabingwa wa jumla katika michuano hiyo ni somo kubwa kwa kila mwanamichezo kuamini wanaweza na kuliwakilisha vyema shirika hata itakapotokea michuano mingine.

Mbali na ubingwa wa jumla TPA ilijinyakulia makombe mengine la mshindi wa kwanza kwenye kikapu wanaume, netboli, bao huku wakipata la mshindi wa tatu kwenye kikapu wanawake.

Hamissi amesema huu ni mwaka wa TPA kwa kila kitu kuanzia majukumu ya kiofisi kuwa na ufanisi mzuri hadi katika michezo.

Michezo ya Shimuta ilifanyika Mkoani Morogoro na kushirikisha zaidi ya timu 40 katika michezo tofauti tofauti kwa wanawake na wanaume.