Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shime na hesabu za vidole Kombe la Dunia U20

Muktasari:

  • Tanzania ilikumbana na kipigo kingine katika Kundi B baada ya kupoteza mechi ya kwanza kwa mabao 5-1 dhidi ya Brazil kabla ya kupokea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya England, lakini Shime alisema kikubwa alichokiona ni mabadiliko ya kiwango ikilinganishwa na mchezo wao wa kwanza, akiamini timu yake inaweza kumaliza kampeni hiyo kwa matokeo mazuri.

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania chini ya miaka 20, Bakari Shime, amesema bado hajakata tamaa na ana imani kuwa timu hiyo ina nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia licha ya Tanzanite kupoteza mechi mbili mfululizo.

Tanzania ilikumbana na kipigo kingine katika Kundi B baada ya kupoteza mechi ya kwanza kwa mabao 5-1 dhidi ya Brazil kabla ya kupokea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya England, lakini Shime alisema kikubwa alichokiona ni mabadiliko ya kiwango ikilinganishwa na mchezo wao wa kwanza, akiamini timu yake inaweza kumaliza kampeni hiyo kwa matokeo mazuri.

Shime alisema tofauti kubwa ilionekana katika namna wachezaji wake walivyocheza, akieleza kuwa katika mchezo wa kwanza walionekana kuwa na hofu na kushindwa kutekeleza maelekezo ya benchi la ufundi.

“Mchezo wa kwanza tulikuwa na majaribio mawili tu ya kufunga, lakini kwenye mchezo huu tumepata majaribio tisa dhidi ya 15 ya wapinzani wetu. Hii inaonyesha kuna mabadiliko,” alisema Shime.

Hata hivyo, kocha huyo alikiri kuwa makosa ya mchezaji mmoja mmoja yaliigharimu Tanzania, hasa baada ya wapinzani kupata penalti mbili ndani ya kipindi kifupi.

Mbali na hilo, Shime alisema safu yake ya ulinzi ilipata changamoto kubwa upande wa kulia wa uwanja, eneo ambalo wapinzani walilitumia vizuri na kufunga mabao yao. Pamoja na kipigo hicho, Shime bado anaimani na timu hiyo akiamini Tanzania inaweza kutumia nafasi ya kufuzu kupitia timu zitakazokuwa na matokeo mazuri miongoni mwa waliomaliza katika nafasi ya tatu.

“Tunatakiwa kuangalia mchezo wetu wa mwisho. Canada pia imepoteza na ina pointi moja, hivyo mchezo huo utakuwa wa muhimu sana. Tukishinda, tutapata pointi tatu ambazo zinaweza kutusaidia,” alisema.

Kwa upande wa beki, Diana Mnally alisema uzoefu wa kucheza Kombe la Dunia umemsaidia kuona tofauti kubwa kati ya mashindano ya U-17 na U-20. Ikumbukwe beki huyo alikuwa miongoni mwa nyota waliocheza Kombe la Dunia la U-17 mwaka 2022 akifunga bao wakati timu hiyo ikifika robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia.

“U-20 ni tofauti kabisa. Hapa tunakutana na wachezaji ambao wamejiandaa vizuri na wengine wamecheza soka la kulipwa nje ya nchi kwa miaka kadhaa, Wao walikuwa na tofauti ndogo ambazo ziliwasaidia kutuzidi, lakini haimaanishi sisi tulikuwa dhaifu tulipambana,” alisema.

Akizungumzia mchezo wa mwisho, Diana alisema utakuwa mgumu kwa kuwa Canada itakuwa ikisaka ushindi baada ya kupoteza mchezo.

Tanzanite Queens itashuka tena dimbani Ijumaa, Septemba 11, 2026 katika mechi ya mwisho dhidi ya Canada na kama itanyakua pointi tatu itafufua matumaini ya kufuzu hatua ya 16 bora.