Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba Queens, Yanga Princess zaanza na ushindi WPL

SIMBA Q Pict

MECHI sita za mzunguko wa kwanza za Ligi ya Wanawake 2026-2027 zilizochezwa leo Oktoba 28, 2026, zimeonyesha namna ambavyo timu za ugenini zilivyoanza kwa kasi.

Simba Queens ambao ni mabingwa watetezi waliokuwa ugenini, waliikabili Kilimanjaro Wonders Queens kwenye Uwanja wa Ushirika uliopo Moshi mkoani Kilimanjaro, ikishinda mabao 3-0.

Dakika 10 tu zilitosha kwa Aisha Mnunka kufungua ukurasa wa mabao, akianza msimu mpya kwa staili ileile aliyomalizia msimu uliopita. Bao hilo liliwapa Simba utulivu, kabla ya Senaf Demise kuongeza bao lingine, kisha wenyeji kujifunga na kuifanya Simba kuondoka na ushindi wa mabao 3-0.

Msimu uliopita Mnunka ndiye aliyekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Bilo Queens, timu iliyopanda daraja, ameonyesha tena uwezo wake wa kuanza ligi kwa kishindo.

Katika mchezo huo wa msimu uliopita, Jentrix Shikangwa ambaye kwa sasa anakipiga FC Masar ya Misri alifunga mabao matatu. Alikuwa na msimu bora uliopita, akifunga mabao 11

Yanga Princess nayo ilikuwa ugenini dhidi ya Bunda Girls kwenye Uwanja wa Karume mkoani Mara, wageni hao waliondoka na ushindi wa mabao 3-0. Mabao ya Cynthia Musungu, Temesgen Mesay na Salamata Kouanda ndio yaliyoipa ushindi wa pointi tatu timu hiyo.

Ushindi wa wageni haukuishia kwa vigogo hao pekee. JKT Queens ilitoka ugenini na kuichapa Geita Queens mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita, wakati Alliance Girls ikiibuka na ushindi kama huo dhidi ya Ceasiaa Queens kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

Bunda Queens nayo ilifanya yake kwa kuifunga Tausi FC mabao 5-2 kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, ushindi ulioifanya mechi hiyo kuwa miongoni mwa iliyokuwa na mabao mengi zaidi katika siku ya ufunguzi.

Fountain Gate Princess nayo ikiwa nyumbani, imepokea kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Mashujaa Queens kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.