Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shekhan aanza kulipa imani Singida, atekeleza ushauri wa mastaa wa Yanga

Muktasari:

  • Na sasa akiwa katika msimu wake wa kwanza Singida Black Stars, kiungo huyo ameanza kulipa imani ya benchi la ufundi kwa kiwango kinachompa nafasi ya kuonekana, akifunga mabao mawili katika mechi nne za mwanzo za Ligi Kuu Bara msimu wa 2026/27.

KUTOKA kuwa mchezaji wa kikosi cha pili cha Yanga hadi kuanza kuonyesha makali akiwa na Singida Black Stars, kiungo Shekhan Khamis anaendelea kujijenga kisoka huku akibeba ushauri wa mabosi na wachezaji wenzake aliowaacha Jangwani.

Na sasa akiwa katika msimu wake wa kwanza Singida Black Stars, kiungo huyo ameanza kulipa imani ya benchi la ufundi kwa kiwango kinachompa nafasi ya kuonekana, akifunga mabao mawili katika mechi nne za mwanzo za Ligi Kuu Bara msimu wa 2026/27.

Shekhan, ambaye alijiunga na Yanga Desemba 2023 akiwa na umri wa miaka 18, amepitia hatua tofauti katika safari yake ya soka, ikiwamo kucheza kikosi cha pili kabla ya kupata nafasi katika timu ya wakubwa. Hata baada ya kuondoka Jangwani kwa mkopo na kuhamia Singida Black Stars kabla ya msimu huu, uhusiano wake na baadhi ya wachezaji wa Yanga haujakatika. Bado wanamfuatilia, wanampongeza anapofanya vizuri na kumpa maelekezo yanayomsaidia kuboresha maeneo ambayo awali yalikuwa yakimpa changamoto.

Miongoni mwa mambo aliyoyabeba kutoka Yanga ni ushauri kuhusu upigaji wa mpira, eneo ambalo sasa linaonekana kuwa sehemu ya maendeleo yake. Lakini zaidi ya mbinu za kucheza, Shekhan anaona kuongezeka kwa kujiamini kuwa mabadiliko makubwa zaidi tangu alipojiunga na Singida, ambako anapata nafasi ya kuonesha uwezo wake katika ligi na michuano ya kimataifa.

YANGA WANAMSHAURI

Ingawa sasa anavaa jezi ya Singida Black Stars, Shekhan hajapoteza mawasiliano na baadhi ya wachezaji aliocheza nao Yanga kwa msimu mmoja na nusu. Ibrahim Bacca na Mudathir Yahya ni miongoni mwa wanaoendelea kumtia moyo, hasa wanapoona akifanya vizuri uwanjani.

“Wananipongeza na kunipigia simu wakiniambia, ‘Sasa hivi umepatia.’ Mwanzoni nilikuwa na tatizo kwenye upigaji wa mpira, wakanishauri na kunielekeza namna ya kufanya mazoezi ya kupiga mpira. Nashukuru Mungu, sasa hivi ninapopata nafasi kwenye mechi napiga na mpira unaingia.”


SAFARI BADO INAENDELEA

Kutoka akademi ya JKU visiwani Zanzibar akiwa na umri wa miaka 11, kupitia timu ya pamoja ya Zanzibar, hadi kujiunga na Yanga Desemba 2023, Shekhan amepitia hatua zinazompa uzoefu wa kuendelea kukua katika soka.

Alianza akiwa na kikosi cha pili cha Yanga kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa na kucheza mechi saba za Ligi Kuu msimu wa 2023/24. Baadaye alihamia Singida Black Stars kwa mkopo, akitafuta muda zaidi wa kucheza na kuendeleza kipaji chake.


MABAO YANA KITU

Msimu wa 2026/27 umeanza kwa matumaini kwa kiungo huyo, ambaye amefanikiwa kufunga mabao mawili katika mechi nne za mwanzo za Ligi Kuu Bara akiwa na Singida Black Stars chini ya kocha Papy Kimoto.

Miongoni mwa mabao hayo ni lile alilofunga dhidi ya Simba, ambalo lilionesha utulivu wake mbele ya lango licha ya timu hiyo kukabiliwa na upinzani mkali, huku kiwango hicho kinampa nafasi ya kuendelea kujitengenezea jina katika kikosi hicho, hasa anapopata dakika za kutosha kucheza.

Mbali na ligi, Shekhan amepata nafasi ya kuonesha uwezo wake katika mashindano ya kimataifa. Aliandika rekodi ya kufunga bao lake la kwanza la kimataifa barani Afrika wakati Singida Black Stars ilipoichapa Al-Ghazala SC ya Sudan Kusini mabao 7-1 katika hatua ya mchujo ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mabao hayo ya mwanzo katika msimu huu ni sehemu ya safari yake ya kutafuta nafasi ya kudumu kikosini. Hata hivyo, anaelewa kuwa anatakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kudumisha kiwango hicho na kuwathibitishia makocha kuwa anaweza kuwa mchezaji muhimu katika mipango ya timu.

MAISHA NDANI YA SINGIDA

Kuhusu mazingira ya klabu yake mpya, Shekhan anasema hajaona tofauti kubwa kati ya Singida Black Stars na Yanga, akieleza kuwa zote ni timu nzuri zinazompa mchezaji mazingira ya kufanya kazi na kuendeleza uwezo wake.

“Kwa kweli tofauti hamna, sijaona tofauti yoyote. Zote ni timu nzuri. Timu niliyotoka ni nzuri, Yanga ni timu nzuri na Singida pia inazidi kuwa nz uri,” an asema.

H a ta hivyo, anasema mabadiliko makubwa kwake yamekuwa katika upande wa kujiamini. Kwa mtazamo wake, kila siku anayoendelea kuc heza na kupata nafasi ya kuonesha uwezo wake inamsaidia kuimarika zaidi.

Anasema: “Kwanza sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu. Mpaka sasa nina hali nzuri na timu yangu mpya. Upepo umekuja vizuri, na kila siku zinavyokwenda nazidi kuwa na kiwango kizuri na confidence. Kitu kilichoongezeka sana ni ujasiri.”

Anasema alipofika Singida alielezwa kuwa anakwenda kwenye timu yenye wachezaji wenye uwezo mkubwa, hivyo alitakiwa kuonesha juhudi zake ili aweze kushindania nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

“Nilipojiunga niliambiwa kwamba ni timu nzuri yenye wachezaji wazuri. Kwa hiyo nilichot akiwa kufanya ni kujituma ili nipate nafasi ya kuanza kwenye timu ya Singida. Nashukuru Mwenyezi Mungu, kila siku nazidi kujituma na kiwango changu kinaonekana,” anasema mchezaji huyo.


USHINDANI NI MKUBWA

Licha ya kuanza vizuri, Shekhan anafahamu kuwa nafasi ya kucheza mara kwa mara haiji kwa urahisi. Singida Black Stars ina wachezaji wenye uwezo mkubwa, hasa katika maeneo ya mbele, jambo linalomlazimu kila mchezaji kupambana ili kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.

Anasema ushindani huo ni sehemu ya maisha ya soka na unawapa wachezaji sababu ya kuendelea kujituma katika mazoezi na wanapopata nafasi ya kucheza.

“Ushindani ni mgumu ukiangalia wachezaji wa mbele waliopo, kwa sababu ni wazuri. Mpaka sasa namshukuru Mungu, kila mtu anapambania nafasi yake na anataka kucheza ili aonekane,” anasema.

KIMATAIFA KUNAMJENGA

Kupata nafasi ya kucheza katika mashindano ya kimataifa ni fursa nyingine ambayo Shekhan anaiona kuwa muhimu katika ukuaji wake kisoka. Anasema timu zinazokutana katika michuano hiyo huwa na ushindani mkubwa, hivyo kila mchezo unampa nafasi ya kujifunza mbinu mpya na kupima uwezo wake dhidi ya wapinzani tofauti.

“Namshukuru Mungu kwa sababu napata nafasi ya kucheza na kuonekana. Katika mashindano ya kimataifa timu zote unazokutana nazo ni ngumu, lakini kila mchezaji anazidi kuongezeka na kiwango kinaendelea kuwa kizuri kila siku.”

TIMU YA TAIFA

Katika upande wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Shekhan amepata nafasi ya kuitumikia Tanzania katika kikosi cha vijana chini ya miaka 23. Anasema mechi walizocheza zilikuwa na changamoto, hasa walipoanza kwa kucheza ugenini ambako walikabiliwa na hali ngumu ya hewa. “Zilikuwa mechi ngumu. Tulianzia ugenini na hali ya hewa pale ilikuwa nzito, tukapoteza kwa mabao 4-1. Tuliporudi nyumbani tulicheza vizuri na tukapata mabao, ingawa hayakutosha kutufanya tupite. Tunamshukuru Mungu, kwa sababu mambo yameendelea kuongezeka tangu mwanzo mpaka sasa,” anasema.


NAMBA 10 NDIO NI ZAIDI

Shekhan ana uwezo wa kucheza nafasi kadhaa uwanjani, jambo linalompa kocha chaguo zaidi katika kupanga kikosi kulingana na mahitaji ya mchezo. Anaweza kucheza kiungo mkabaji, namba sita, kiungo wa kati namba nane, kiungo mshambuliaji namba 10 na winga wa kulia.

“Ninaweza kucheza nafasi za mbele kuanzia namba sita, namba nane, namba 10 ndiyo namba yangu, na winga wa kulia. Namba tisa siwezi kucheza.”


CHASAMBI, PIPINO NA MALICK

Nje ya uwanja, Shekhan anaeleza kuwa ana ukaribu na baadhi ya wachezaji wa Singida Black Stars, akiwataja Chasambi, Pipino na Malick kuwa miongoni mwa marafiki zake.

Anasema hupenda kuwa nao, ingawa Malick ndiye anayemchukulia kuwa mkorofi zaidi katika kundi hilo kwa namna anavyomchokoza. Tofauti na anavyokuwa uwanjani, ambako anatakiwa kupambana na ushindani wa soka, Shekhan anasema nje ya uwanja ni mtu mpole anayependelea maisha ya utulivu.

“Nje ya uwanja mimi ni mtu mpole, napenda kulala na sina mambo mengi, yupo mchezaji wa karibu sana ambaye ananichukua tunaenda mazoezini, na ananipa sapoti kubwa mpaka sasa hivi,” anasema.