Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shalulile na Mudathir waendeleza rekodi ya ushindi

YANGA Pict

Muktasari:

  • Aziz KI aliyerejea Yanga msimu huu baada ya kuachana na Al-Ittihad ya Libya, jana katika mechi dhidi ya Fountain Gate ambayo Yanga ilishinda 2-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, alitumika kwa dakika 66, kisha akampisha Albert Kangwanda.

DAKIKA 66 alizocheza Stephane Aziz KI katika mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara tangu arejee Yanga, zimekuwa nzuri upande wake na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo wasiwe na dukuduku la kutoa kwani ilikuwa ikisubiriwa atafanya nini.

Aziz KI aliyerejea Yanga msimu huu baada ya kuachana na Al-Ittihad ya Libya, jana katika mechi dhidi ya Fountain Gate ambayo Yanga ilishinda 2-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, alitumika kwa dakika 66, kisha akampisha Albert Kangwanda.

Katika dakika hizo 66, Aziz KI ndiye aliyehusika katika bao la kwanza lililofungwa na Peter Shalulile dakika ya 26, baada ya kutoa asisti ya kiufundi kwa kisigino.

Aziz KI mbali na asisti hiyo, alifanya matukio kadhaa ya faida, akipiga mashuti matatu likiwemo moja lililogonga mwamba, lingine likilenga lango na moja likizuiwa na mabeki wa Fountain Gate.

Kiungo huyo raia wa Burkina Faso, aliondoka Yanga Juni 2025 akitimkia Wydad Casablanca ya Morocco, alipodumu hadi Januari na kusaini Al-Ittihad alikokaa pia miezi sita akarejea Yanga.

YANG 02

Mechi yake ya mwisho Aziz KI kucheza Yanga kabla ya kurejea, pia ilikuwa ugenini, lakini wakati huo ilikuwa ni nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya JKT Tanzania, Yanga ikishinda 2-0 iliyochezwa Mei 18, 2025 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Baada ya mechi hiyo akaaga.


MECHI ILIVYOKUWA

Katika mechi ya jana ambayo Yanga imeendeleza ushindi kwa asilimia mia moja, vinara hao wa Ligi Kuu Bara na mabingwa watetezi, hawakuanza kama ambavyo mashabiki wamezoea kuona kwenye mechi zilizopita, baada ya Kocha Mkuu, Manqoba Mngqithi kufanya mabadiliko kadhaa kikosi cha kwanza, akiwamo beki wa kati Farouk Komara aliyeanza akichukua nafasi ya Bakari Mwamnyeto aliyekuwa akicheza mara kwa mara nafasi hiyo msimu huu.

Kitaalamu, mabadiliko hayo yalionekana kuwa na lengo la kuongeza nguvu kwenye ujenzi wa mashambulizi kutoka nyuma, huku Yanga ikijaribu kutumia pasi fupi na za haraka badala ya kutegemea mipira mirefu. Komara akiwa beki wa kati, alipewa jukumu la kusaidia kuanzisha mashambulizi, huku viungo wakishuka kumpa chaguo la pasi.

YANG 01

Upande wa Fountain, walikuwa na mpango wa kuizuia Yanga kucheza kwa uhuru, lakini mambo ni kama yangewaendea vibaya mapema dakika ya tisa baada ya mshambuliaji wao Chukwunonye Obasi kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi Amina Kyando, kabla ya kuibadili na kumpa ya njano kuashiria faulo aliyomfanyia Ibrahim Bacca haikustahili adhabu hiyo, hivyo Fountain Gate ikaendelea na idadi yake kamili ya wachezaji.

Licha ya tukio hilo kuvuruga kwa muda mpangilio wa mechi, Yanga iliendelea kutawala zaidi mpira na kusogea eneo la Fountain Gate.

Siri kubwa ilikuwa namna ilivyokuwa ikitumia maeneo ya pembeni na kuingiza mipira katika eneo la hatari, huku Peter Shalulile akifanya kazi ya kuvuta mabeki na kutafuta nafasi kati ya mabeki wa katina dakika ya 26, mpango huo ukazaa matunda kwa bao hilo la Shalulile.

Kwa Shalulile, hilo ni bao la tatu kwenye ligi tangu atue Yanga akicheza mechi tano, akifikia rekodi yake ya mabao aliyofunga Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu uliopita akiwa na Mamelodi Sundowns alipocheza mechi 13. Aziz KI hiyo kwake ilikuwa asisti ya kwanza.

Hadi mapumziko, Yanga ilikuwa imepata faida ya bao moja, lakini mabadiliko ya kikosi yalionyesha benchi la ufundi lilikuwa likitafuta suluhisho tofauti.

YANG 03

Wakati kipindi cha pili kinataka kuanza, Manqoba alimtoa Cheikh Toure, nafasi yake ikachukuliwa na Selemani Mwalimu, huku pia Salum Abubakar ‘Sureboy’ akimpisha Mudathir Yahya, mabadiliko yaliyolenga kuongeza nguvu na ufanisi eneo la mbele na kiungo.

Mabadiliko hayo yaliinufaisha Yanga kwani dakika ya 76, Mudathir alifunga bao la pili kwa kichwa akimalizia mpira uliookolewa na kipa Rashid Parapanda aliyejaribu kuzuia shambulizi la Mwalimu. Hilo ni bao la pili kwa Mudathir kwenye ligi msimu huu.

Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 15 baada ya kushinda mechi zote tano za kwanza, ikifunga mabao 15 na kuruhusu mawili pekee hali iliyomfanya kipa Djigui Diarra kufikisha clean sheet tatu.

Yanga mabao yake 15 iliyofunga, imeyagawa vizuri na manane ni kipindi cha kwanza na saba kipindi cha pili.