Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saa 72 zampa mtihani Juma Mgunda

MGUNDA Pict

Muktasari:

  • Mgunda amesema muda uliopo kati ya mechi hizo mbili ni mfupi sana kwa timu kufanya maandalizi ya kutosha, hasa kwa kuzingatia mahitaji ya wachezaji kupata muda wa kurejesha nguvu baada ya mchezo mmoja kabla ya kuingia mwingine.

KOCHA Mkuu wa Namungo FC, Juma Mgunda, ameingiwa na hofu juu ya ratiba ya Ligi Kuu Bara inayowakabili baada ya kikosi hicho kucheza Agosti 29, 2026 jijini Dar es Salaam dhidi ya JKT Tanzania, kisha kutakiwa kushuka dimbani kesho Jumanne mkoani Singida dhidi ya wenyeji wao Singida Black Stars. Kutoka mechi moja kwenda nyingine ni takribani siku tatu ambazo ni sawa na saa 72.


Mgunda amesema muda uliopo kati ya mechi hizo mbili ni mfupi sana kwa timu kufanya maandalizi ya kutosha, hasa kwa kuzingatia mahitaji ya wachezaji kupata muda wa kurejesha nguvu baada ya mchezo mmoja kabla ya kuingia mwingine.

“Mechi hizi ni ngumu mno, kama sasa hivi sidhani kama nitapata hata masaa 72, lakini utaona kabisa kuna kazi ya kufanya,”  amesema Mgunda akieleza ukubwa wa changamoto hiyo.

MGU 01

Mgunda alikiri kuwa, katika mechi dhidi ya JKT Tanzania, kikosi chake kilitengeneza nafasi kadhaa lakini kikashindwa kuzitumia, huku makosa madogo yakigeuka kuwa moja ya sababu iliyowafanya wapoteze mchezo huo.

MGU 02

Mgunda amesema hataki kuitumia ratiba kama kisingizio, bali kufanya marekebisho muhimu na kuandaa mpango mkakati utakaowapa nafasi ya kupambana na Singida Black Stars.

“Kazi ipo, lakini tutajipanga ili kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya timu nzuri,”  ameongeza Mgunda.

Namungo ambayo leo inaingia uwanjani kukabiliana na Singida Black Stars, mechi iliyopangwa kuchezwa Uwanja wa Airtel kuanzia saa 1:00 usiku, rekodi zinaonyesha timu hizo zimekutana jumla ya mara kumi, Singida ikishinda nne, Namungo tatu, huku sare zikiwa tatu.