Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti yapangwa na Kenya kufuzu AFCON

Muktasari:

  • Droo hiyo iliyofanyika leo Septemba 23, 2026 jijini Dar es Salaam, iliendeshwa na Meneja wa Mashindano wa CECAFA, Yusuf Mossi, akisaidiwa na kiungo wa Singida Black Stars, Ladaki Chasambi, ambaye alipewa nafasi hiyo kutokana na kuwa sehemu ya wachezaji waliowahi kufanya vizuri kwenye mashindano ya vijana ya CECAFA.

TIMU ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, imepangwa Kundi C pamoja na Kenya na Djibouti katika kuwania tiketi ya Ukanda wa CECAFA kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U-17) mwaka 2027.

Droo hiyo iliyofanyika leo Septemba 23, 2026 jijini Dar es Salaam, iliendeshwa na Meneja wa Mashindano wa CECAFA, Yusuf Mossi, akisaidiwa na kiungo wa Singida Black Stars, Ladaki Chasambi, ambaye alipewa nafasi hiyo kutokana na kuwa sehemu ya wachezaji waliowahi kufanya vizuri kwenye mashindano ya vijana ya CECAFA.

Tanzania inaingia kwenye mashindano hayo ikiwa na kumbukumbu nzuri baada ya kutwaa ubingwa wa CECAFA U-17 mwaka 2025 nchini Ethiopia, ilipoifunga Uganda mabao 3-2 katika fainali. Ushindi huo uliifanya Tanzania kumaliza mashindano ikiwa imeshinda mechi zote sita ilizocheza.

Katika safari ya kuelekea ubingwa huo, Tanzania ilionyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao, ikiwemo ushindi wa 11-0 dhidi ya Djibouti ambapo Luqman Mbalasalu alifunga mabao sita. Pia iliifunga Uganda 2-1 kwenye hatua ya makundi.

Katika nusu fainali, Tanzania iliifunga Kenya mabao 3-1 na kuwa timu ya kwanza kutoka CECAFA kufuzu Fainali za AFCON U-17 2026, kisha ikaifunga Uganda 3-2 katika mchezo wa mwisho wa mashindano.

Kenya, ambayo sasa imepangwa tena na Tanzania, ilimaliza safari yake ya mwaka huo kwa kufungwa na Ethiopia katika mchezo wa kutafuta nafasi ya tatu.

Kwa droo hiyo, Rwanda imepangwa Kundi A pamoja na Sudan, Somalia na Sudan Kusini, wakati Uganda ipo Kundi B sambamba na Ethiopia na Burundi.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Kigali nchini Rwanda, kuanzia Oktoba 10 hadi 19, 2026 huku timu tatu bora zikifuzu AFCON U-17 mwaka 2027.