Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Yanga anukia Sauzi


KOCHA Msaidizi wa Yanga, Simo Dladla huenda akarejea Afrika Kusini ili kukifundisha kikosi cha Richards Bay FC, baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, raia wa Bulgaria Dimitar Pantev kuondoka kutokana na mwenendo mbaya katika msimu huu.


Taarifa kutoka Afrika Kusini, zinadai Dladla ni miongoni mwa makocha wanaopendekezwa kuchukua nafasi ya Pantev aliyewahi kuifundisha Simba, aliyeondolewa kutokana na mwenendo usioridhisha katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini tangu msimu umeanza.

Dladla aliyejiunga na Yanga akiwa Kocha msaidizi wa Manqoba Mngqithi aliyeondoka Oktoba 24, 2026, anaweza kuondoka pia kikosini humo, baada ya ujio wa Kocha Mkuu, Fadlu Davids aliyekuja na msaidizi mpya wa benchi la ufundi, Darian Wilken.

Kocha huyo aliwahi kufanya kazi na Richards Bay FC kati ya mwaka 2020 hadi 2021, jambo linalowafanya mabosi wa timu hiyo kuanzisha mpango wa kumrejesha tena kikosini, kwa lengo la kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mbulgaria Dimitar Pantev.

Pantev aliyewahi kuifundisha Simba kuanzia Oktoba 3, 2025, kisha kudumu kwa siku 60, baada ya kuondoka Desemba 2, 2025, ameiongoza Richards Bay FC katika mechi tatu za Ligi Kuu ya Afrika Kusini bila ya ushindi wowote kufuatia kuchapwa zote.

Kocha huyo aliiongoza Richards Bay FC ikianza na kichapo cha mabao 4-1, dhidi ya Mamelodi Sundowns FC, ikachapwa tena 3-1, dhidi ya Shekhekhune United, kisha ikaendeleza mwenendo mbaya baada ya kuchapwa pia mabao 3-1 na Kruger United FC.

Dladla ana uzoefu mkubwa baada ya kufundisha timu mbalimbali za AmaZulu FC akiwa msaidizi wa Kocha Mkuu, Arthur Zwane, Durban City FC zamani Maritzburg United FC, Uthongathi FC, Richards Bay FC na Golden Arrows zote za kwao Afrika Kusini.