Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sasii afungiwa miezi sita, Fadlu, Sowah nao yawakuta

Muktasari:

  • Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Usimamizi wa Ligi imesema Sasii amekumbana na adhabu hiyo baada ya kuwa na makosa mengi yaliyotafsirika kushindwa kumudu mchezo huo ambao Simba ilishinda kwa bao 1-0.

Mwamuzi Herry Sasii amekumbana na adhabu Kali, baada ya kufungiwa miezi sita kwa makosa ya kushindwa kutafsiri Sheria kwenye mchezo kati ya Simba na Singida Black Stars.

Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Usimamizi wa Ligi imesema Sasii amekumbana na adhabu hiyo baada ya kuwa na makosa mengi yaliyotafsirika kushindwa kumudu mchezo huo ambao Simba ilishinda kwa bao 1-0.

Mbali na Sasii kocha wa Simba Fadlu Davids amekumbana na adhabu Kali akitozwa Faini ya sh 2 Milioni kwa makosa ya kushambulia Bodi ya Ligi kwa tuhuma alizozitoa.

Naye msaidizi wa Kocha huyo Reidoh Berdien amefungiwa mechi tatu sambamba na Faini ya sh 1 Milioni kwa kosa la kuanzisha vurugu, baada ya kudaiwa kurusha Koni kwenye benchi la Singida.

Mshambuliaji wa Singida Jonathan Sowah naye ametozwa Faini ya sh 1 Milioni kwa kosa la kuwaonyesha mashabiki wa Simba ishara ya matusi sambamba na kung'oa kibendera

Kule Mashujaa nako Kuna adhabu mbili Kali ambapo mshambuliaji Seif Karihe amesimamishwa kwa kwa mechi tatu akitozwa na Faini ya sh 500,000 kwa kosa la kurusha chupa ya maji kwenda kwa mashabiki, wakati timu yake ikicheza ugenini dhidi ya Simba.

Mtunza wa vifaa wa Mashujaa Juma Nyenje amefungiwa kwa miezi sita pia akitozwa Faini ya sh 500,000 kwa kosa la kurusha chupa ya maji kwenda kwa mashabiki kwenye mchezo huo huo.