Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samatta na chama lake mambo magumu Ufaransa

Muktasari:

  • Katika msimu huu wa 2026/2027, Samatta amecheza katika michezo 11 ya Ligi Kuu Ufaransa, akianza kikosi cha kwanza katika michezo tisa huku akitokea benchi katika michezo miwili.

MCHEZAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anapitia kipindi kigumu pamoja na timu yake ya Le Havre, inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ufaransa, ‘Ligue 1’ kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya wanayopata katika mechi za ligi hiyo.

Katika msimu huu wa 2026/2027, Samatta amecheza katika michezo 11 ya Ligi Kuu Ufaransa, akianza kikosi cha kwanza katika michezo tisa huku akitokea benchi katika michezo miwili.

Nahodha huyo wa zamani wa Taifa Stars, amefunga mabao mawili pekee tangu msimu ulipoanza, lakini amekosa mwendelezo mzuri wa kufunga tangu alipofanya hivyo Septemba 19, 2026 alipofunga bao katika mechi dhidi ya Toulouse.

Msimu huu Samatta alianza kwa kuonyesha kiwango bora baada ya kupachika bao katika mechi ya kwanza dhidi ya Olympique Lyon, kisha akafunga lingine tena katika mchezo wa nne dhidi ya Toulouse.

Mabao hayo yanamfanya nyota huyo wa Tanzania kufikisha idadi ya mabao manane katika Ligi Kuu ya Ufaransa tangu alipojiunga na Le Havre, Agosti 2025.

Hata hivyo, mambo yanaonekana kuwa magumu kwani hadi sasa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33 hajaingia wavuni katika mechi sita mfululizo huku timu yake nayo ikiendelea kudondosha pointi tatu kwa wapinzani. Le Havre hadi sasa imecheza michezo 11 ya Ligi Kuu bila kupata ushindi wowote ikiambulia sare mara mbili na kukubali vipigo tisa huku ikiburuza mkia katika msimamo wa ligi wenye timu 18.

Timu hiyo pia imefungwa mabao 25 huku yenyewe ikifunga 10 na itashuka tena dimbani Jumamosi, Novemba 28 dhidi ya Strasbourg.