Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samatta kupewa viatu vya Kane pale Tottenham

Muktasari:

  • Spurs mara kadhaa imekuwa ikipitia kipindi kigumu pale Kane anakuwa amepata majeraha hivyo humlazimu kocha wa timu hiyo, Muargentina, Pochettino kumtumia Mkorea Kusini, Son Heung-Min ambaye sio mshambuliaji wa kati kiasili.

UTAMU kunoga. Imeanza kutajwa kuwa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta anaweza kutua Tottenham Hotspur baada ya kuzagazaa kwa taarifa za mshambuliaji wa timu hiyo, Harry Kane kuwa na mpango wa kutimka mwishoni mwa msimu.

Kinachotajwa kuwa kinaweza kumuondoa Kane Spurs ni ukame wa mataji kwenye klabu hiyo ambayo msimu huu klabu yake imeanza kutoka kwenye mbio za ubingwa kutokana na kupoteza pointi katika michezo muhimu.

Aidha kocha wa timu hiyo, Mauricio Pochettino hivi karibuni alisema Spurs inahitaji miaka mitano au 10 kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Hata hivyo, tangu Januari wakati wa dirisha dogo, Spurs ilikuwa ikihusishwa na kuihitaji hudumu ya Samatta ambaye ni kinara wa mabao Ligi Kuu Ubelgiji ili akakiongezee nguvu kikosi hicho kwenye safu yake ya ushambuliaji ambayo imekuwa ikimtegemea Kane peke yake.

Spurs mara kadhaa imekuwa ikipitia kipindi kigumu pale Kane anakuwa amepata majeraha hivyo humlazimu kocha wa timu hiyo, Muargentina, Pochettino kumtumia Mkorea Kusini, Son Heung-Min ambaye sio mshambuliaji wa kati kiasili.

Yote hiyo imetokana na Fernando Llorente ambaye ni mbadala wa Kane kushindwa kufanya kweli pindi apopata nafasi ya kucheza, Mhispania huyo amepachika bao moja tu msimu huu kwenye michezo 13 ya Ligi Kuu England.

Hofu ya kuondoka kwa Kane mwishoni mwa msimu imeanza kuwafanya vigogo wa Spurs kuhaha kwa kuangalia uwezekano wa kumnasa Samatta ambaye ni miongoni mwa washambuliaji wanaofanya vizuri kwa sasa Ulaya.

Katika michezo 26 ya Ligi Kuu Ubelgiji maarufu kama Jupiler Pro, Samatta ameifungia klabu yake ya KRC Genk mabao 20.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Fox, Real Madrid iko tayari kumwachia Gareth Bale ili imjumuishe kundini Harry Kane mwenye mabao 16 Ligi Kuu England.

IBRAHIMOVIC ACHOCHEA MOTO

Nyota wa zamani wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic anayeichezea LA Galaxy ya Marekani, amesema umefika muda wa Kane kuondoka Spurs na kujiunga na klabu kubwa zaidi ili aweze kushinda mataji.

Kane ambaye ni nahodha wa Timu ya Taifa ya England amefunga jumla ya mabao 123 kwenye michezo 173 ya Ligi Kuu England, hajawahi kutwaa taji lolote akiwa na Spurs.

“Nilipokuwa England, nilimuona akicheza, ni mshambuliaji mzuri ambaye kiwango chake kinaendelea kukua.

“Umefika muda wa kushinda mataji sidhani kama ni sahihi kwake kuendelea kucheza Tottenham ili ajiwekee heshima,” Zlatan alimjibu mwandishi wa Metro, Bethard.