Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salehe Karabaka, Pamba Jiji freshi

KARABAKA Pict

Muktasari:

  • Karabaka aliichezea JKT Tanzania kwa mkopo akitokea Simba aliyojiunga nayo dirisha dogo la Januari mwaka 2024, akitoka JKU SC ya visiwani Zanzibar, kutokana na ufinyu wa nafasi ya kucheza pia mara kwa mara katika kikosi hicho cha Msimbazi.

TAARIFA kutoka Pamba Jiji, zinaeleza, klabu hiyo ipo katika hatua za mwisho za kumsajili kiungo mshambuliaji, Salehe Karabaka, baada ya mkataba wake wa mkopo wa msimu mmoja kutokea Simba kumalizika msimu wa 2025-2026.

Karabaka aliichezea JKT Tanzania kwa mkopo akitokea Simba aliyojiunga nayo dirisha dogo la Januari mwaka 2024, akitoka JKU SC ya visiwani Zanzibar, kutokana na ufinyu wa nafasi ya kucheza pia mara kwa mara katika kikosi hicho cha Msimbazi.

Taarifa kutoka uongozi wa timu hiyo, umeliambia Mwanaspoti, Karabaka amefikia makubaliano na kikosi hicho kwa ajili ya kukitumikia kwa msimu wa 2026-2027, baada ya kuridhishwa na kiwango chake.

KARAB 01

“Makubaliano binafsi tumeshakubaliana na muda wowote kuanzia sasa atasaini mkataba wa mwaka mmoja wa kucheza Pamba Jiji, ni mchezaji mzuri aliyependekezwa na benchi letu la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza,” kilisema chanzo hicho.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Pamba, Ezekiel Ntibikeha, amesema mchakato wa kutangaza wachezaji wote ambao wamefikia makubaliano ya kukichezea kikosi hicho umeanza, baada ya kupitia vizuri ripoti yote ya benchi la ufundi.

“Tumeanza kutangaza wachezaji wapya tukianza na kipa, Steve Ochieng aliyetokea Shabana FC ya kwao Kenya, tutaendelea na wengine kadri tutakavyokuwa tunafikia makubaliano, huu ni muda wa usajili hivyo tuendelee na subra,” amesema Ntibikeha.

KARAB 02

Karabaka alishika nafasi ya pili kwa kufunga mabao mengi ya Ligi Kuu Bara katika kikosi cha JKT Tanzania kwa msimu wa 2025-2026, akiwa nayo manane, nyuma ya mshambuliaji mwenzake nyota, Paul Peter Kasunda aliyefunga tisa.

Akiwa Simba, aliifungia bao moja la Ligi Kuu, katika ushindi wa timu hiyo wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, Mei 3, 2024, kisha baada ya hapo akajiunga na Namungo FC Januari mwaka 2025 na msimu wa 2024-2025, alikifungia mabao mawili.