Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dakika 450 za vita ya siri!

USHINDANI Pict


KUNA vitu vinavyoongeza mvuto Ligi Kuu Bara kwa hatua ilipofikia, kutokana na takwimu za wachezaji zilivyo kwa sasa, kupishana bao moja, wapo wanaolingana mabao, asisti na ‘cleansheets’, jambo linalochochea ushindani mkali zaidi.


Ligi Kuu Bara kwa sasa imebakiza michezo mitano tu ili imalizike na kila timu inatakiwa kuchanga karata zake vizuri kwa kuwa zina malengo tofauti, lakini pia wachezaji nao kila mmoja ana kile anachofikiri kukifanya mwishoni mwa msimu, kuna wachezaji wanaamini kuwa wanaweza kumaliza kileleni kwenye chati ya wafungaji, wengine wanataka kumaliza wakiwa na pasi nyingi zilizosababisha mabao yaani asisti na wengine wanataka kuhakikisha wanamaliza bila timu zao kuruhusu mabao.


Kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), zinaonyesha data za wachezaji kile walichokifanya hadi iliposimama wiki mbili kupisha kalenda ya Fifa.

MTEG 01
MTEG 01

Kwa takwimu hizi inaonekana kuwa kila timu inataka kutumia dakika 450 zilizobaki kujiweka sawa, huku kikuwa na wachezaji ambao takwimu zao zimelingana na wengine, huku wengine wakitofautiana kwa bao moja, pasi moja ya bao kuonyesha kuwa kuna kila dalili kuwa msimu huu mwishoni utakuwa na vita kubwa.


Feisal Salum vs Allan Okello

Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ yeye anakwenda kwenye michezo ya mwishoni mwa msimu akiwa kinara wa mabao baada ya kufunga 14, lakini hapo hapo ameshatoa pasi nane za mabao yaani asisti hii ina maana kuwa ndiye mchezaji ambaye amekuwa na msaada mkubwa zaidi kwenye timu yake msimu huu, lakini anakutana na upinzani mkubwa kutoka kwa kiungo wa Yanga Allan Okello mwenye mabao 11 na pasi saba.

Hali hii inaonyesha kuwa kama Feisal atachanga karata zake vizuri kwenye michezo mitano iliyobaki, ataibuka mfungaji bora lakini pia kuwa kinara wa pasi za mabao asisti, lakini kama atacheza kidogo au kuikosa michezo miwili kati ya mitano iliyobaki anaweza kupitwa na Okello ambaye amehusika kwenye mabao mawili na zaidi kwenye kila mchezo kati ya mitano ya mwisho. Kutokana na mwenendo wa Yanga wa kufunga mabao mengi kwenye kila mchezo, Feisal anatakiwa kufanya kazi kubwa zaidi.

MTEG 02

Elie Mpanzu vs Duke Abuya vs Clatous Chama

Mpanzu anaonekana kukimbizana na Feisal kwenye chati ya vinara wa kupiga pasi za mwisho kila mmoja akiwa na pasi nane lakini anatakiwa kufanya kazi kubwa kutokana na upinzani anaokutana nao kutoka kwa Duke Abuya ambaye naye anazo nane ukiwa ni msimu ambao amefanya kazi kubwa zaidi Yanga, lakini pia anakimbizana na Chama mwenye asisti sita na mabao manane.

Kinachoweza kuwashtua wengi hapa ni kwamba Chama ameonekana kuwa na kasi kubwa zaidi kwenye michezo ya mwishoni na pasi zake hizo amezipiga tangu alipojiunga na Simba akitokea Singida, hapa kunaonyesha kuwa kuna mvutano mkubwa zaidi kwenye michezo hii mitano kwa wale ambao wanataka kuweka rekodi zao sawa na haitashangaza kama kuna mmoja atatoka nyuma na kuwapiku.

MTEG 03

Mabao tisa ni vita

Kuna vita pia ya wachezaji waliofunga mabao manane hadi tisa ambao kwenye takwimu za kawaida wanaonekana kuwa wanaweza kupambana kwenye michezo mitano ya mwisho na kumaliza wakiwa wafungaji bora kwa wastani wa mabao mawili au moja kwenye kila mchezo.

Hawa ni Mossi Ndumumwe(Singida BS), Prince Dube (Yanga) ambao kila mmoja amefunga mabao tisa, shaka hapa ni kwamba kila mchezaji kwenye michezo mitano ijayo atakuwa na kazi kubwa zaidi ya kupambana kuhusu timu kuliko kupambana mwenyewe, Dube ambaye pia ana pasi nne za mabao atalazimika kuipambania Yanga ili ifanikiwe kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa sasa ikiwa na pointi 60 kileleni mbili mbele ya Simba yenye pointi 58, huku  Mossi ambaye hana asisti akipambana kuhakikisha Singida inamaliza kwenye nafasi nne za juu kwa sasa ikiwa na pointi 41 zikiwa ni pointi tatu tu mbele ya JKT Tanzania waliopo nafasi ya tano hivyo wanatakiwa kuchanga karata zao vizuri ili kumaliza msimu wa pili wakiwa kwenye nne bora.

Wenye mabao manane ni Selemani Mwalimu (Simba),Iddy Seleman (Azam), Paul Peter, Saleh Karabaka(JKT Tanzania), Mudathir Yahya (Yanga), Fabrice  Ngoy (Namungo) na Clatous Chota Chama.

MTEG 04

Makipa ni vita

Msimu uliopita Moussa Camara aliibuka kuwa kinara wa cleansheets, akimshinda kipa wa Yanga Djigui Diarra, lakini kwa sasa staa huyo wa Mali kama vile hataki tena dharau kwani tayari ndiye kinara wa clean Sheet akiwa nazo 13, akiwa anakutana na upinzani mkali kutoka kwa Mahamadou Kassali wa Simba ambaye anazo 12 nafasi ya tatu inashikwa na kipa bora wa zamani kwenye ligi Aishi Manula wa Azam aliye nazo 11.

Hii ina walazimisha makipa hawa kuzitaka mechi zao zote zilizobaki, lakini pia kuhakikisha timu zao haziruhusu mabao ili kuwa kipa bora mwishoni mwa msimu kutokana na kanuni za ligi. Hata hivyo mtihani hapa ni kwamba kuna mchezo wa Yanga vs Azam yaani Manula vs Diarra ambao unaonekana kuwa una asilimia kubwa ya kuwa na mabao, lakini pia Simba vs Singida nao unaweza kumtibulia kipa Kassali kutokana na historia ya timu hizo.

MTEG 05

KAULI ZA WACHEZAJI

Mshambuliaji wa Prisons, George Mpole amesema:”Kuna morali inakuwa inapanda kwa mchezaji inapotokea kunakuwa na ushindani wa kufunga mabao mengi iliwahi kutokea kwangu na aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele msimu wa 2021/22, nilimaliza na mabao 17 yeye 16 tulicheza kwa presha kubwa ya mashabiki hadi mechi ya mwisho, awamu wachezaji wengi tumelingana mabao, hiyo inaongeza chachu ya kujituma zaidi.”

Kwa upande wa Edgar Williams wa Dodoma Jiji amesema:”Ingawa jambo la kwanza inakuwa ni malengo ya timu, lakini tunaposhindana kwenye kufunga na tukalingana mabao wachezaji wengi inaongeza morali ya kujituma kwa bidii.”

Kipa wa Pamba, Yona Amosi aliyegongana ‘cleasheets’ saba na kipa  Erick Johola wa Mashujaa amesema:”Hatua ilipofikia ligi, kila mchezaji anakuwa anapambana kwa ajili ya timu ili kufikia malengo, ingawa kama mchezaji nakuwa natamani  kuandika rekodi mpya kila msimu itakayonipa heshima na thamani.”

Ligi Kuu Bara inatarajiwa kumalizika Juni 30, 2026 ambapo bingwa atafahamika.