Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rupia akomalia mawili KenGold FC

RUPIA Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Rupia amesema bado timu hiyo haina balansi nzuri katika eneo la kujilinda na la ushambuliaji, japo, miongoni mwa jambo linalompa matumaini ni jitihada zaidi zinazoendelea kuonyeshwa na kundi kubwa ambalo ni vijana.

BAADA ya mwenendo usioridhisha wa kikosi cha KenGold FC, kocha mkuu wa timu hiyo, Hussein Rupia, amesema kwa sasa kazi kubwa anayoendelea kupambana nayo ni ya kutengeneza balansi katika maeneo muhimu mawili ya kujilinda na ushambuliaji.

Akizungumza na Mwanaspoti, Rupia amesema bado timu hiyo haina balansi nzuri katika eneo la kujilinda na la ushambuliaji, japo, miongoni mwa jambo linalompa matumaini ni jitihada zaidi zinazoendelea kuonyeshwa na kundi kubwa ambalo ni vijana.

“Timu hii ina vijana wengi ambao wanahitaji muda zaidi kuzoeana, nashukuru jitihada ambazo wanaendelea kuzionyesha hadi sasa kwa sababu sio rahisi kutokana na uchanga wao kikosini ingawa, tunaendelea kufanyia kazi taratibu,” amesema Rupia.

Rupia aliyejiunga na KenGold FC akitokea Stand United ya Shinyanga, huku akiwahi kuifundisha pia Hausung FC ya Njombe, amesema licha ya kuifundisha timu hiyo kwa mara ya kwanza msimu huu, ila sio mgeni wa ushindani na Ligi ya Championship.

Kabla ya Rupia timu KenGold ilikuwa chinia ya Jumanne Challe  ambaye amejiunga na Polisi Tanzania. KenGold katika mechi 10, imeshinda tatu tu, sare pia tatu na kupoteza nne, ikifunga mabao 12 na kuruhusu 14, ikiwa nafasi ya 11 na pointi 12.