Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Risasi yaanza vizuri ligi ya kikapu Shinyanga

Muktasari:

  • Ligi hiyo inayodhaminiwa na the Levels by 101, inashirikisha timu ya  B4 Mwadui, Risasi, Kahama Sixers na Veta.

RISASI imeendeleza ubabe wake kwa Kahama Sixers baada ya kuifunga pointi 87-60, katika Ligi ya kikapu ya Mkoa wa Shinyanga, kwenye Uwanja wa Risasi.

Ligi hiyo inayodhaminiwa na the Levels by 101, inashirikisha timu ya  B4 Mwadui, Risasi, Kahama Sixers na Veta.

Katika mechi hiyo, Risasi iliongoza robo tatu za kwanza, kwa pointi 22-18, 18-10,  26-9 na robo ya tatu Kahama Sixers ikapata pointi 23-21.

Kwa upande wa ufungaji, Denisi Bilame wa timu ya Risasi alifunga pointi 24 akifuatiwa na John Samweli aliyefunga pointi 20.

Upande wa timu ya Kahama Sixers alikuwa  Julias George aliyefunga pointi 31, akifuatiwa na Stanslaus  Kabeto aliyefunga pointi 8.

Kamishina wa ufundi na mashindano wa Ligi ya kikapu mkoa wa Shinyanga George Simba, alisema  mfumo utakaotumika ni wa kila timu kucheza nyumbani na ugenini.

Akiongeza kuwa , timu itakayoshika nafasi ya kwanza katika Ligi hiyo, itacheza na ya nne, ya pili na ya tatu, na kila timu itacheza michezo mitatu “best of three pray off”.

Mara ya mwisho zilivyokutana   katika fainali  ya mwaka jana,timu ya Risasi iliifunga Kahama sixers katika michezo 2-1.