Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Raskazone yaipigia hesabu kali KMKM

RASKAZON Pict

Muktasari:

  • Raskazone iliyopanda daraja msimu huu, ilianza Ligi Kuu Zanzibar kwa matokeo ya 0-0 dhidi ya Fufuni, kisha kuichapa Mwenge 2-1, hivyo imerejea Unguja ikiwa na pointi nne.

Raskazone imesema licha ya ugeni wao kwenye Ligi Kuu Zanzibar, lakini bado wanaendelea kujiimarisha ili kupata matokeo mazuri dhidi ya KMKM.

Hayo yameelezwa na Ofisa Habari wa Raskazone, Kazija Thabit wakati akizungumza na Mwanaspoti kabla ya mechi hiyo inayotarajiwa kupigwa Septemba 27, 2026.

Kazija amesema Raskazone imelenga kufanya vizuri katika mechi hiyo, hivyo watahakikisha wanashinda.

"Tunawaheshimu wapinzani wetu kwani wao ni wakongwe wa ligi, lakini hatujawahi kuwa waoga, naamini tutashinda mechi hiyo," amesema.

Amesema baada ya kuvuna pointi nne ugenini wakiwa kisiwani Pemba, sasa wamerudi nyumbani Unguja kuendeleza mapambano yao.

Kazija amesema makocha wanaendelea kufanyakazi ya kuwaandaa wachezaji na kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mechi mechi mbili walizocheza kisiwani Pemba.

Raskazone iliyopanda daraja msimu huu, ilianza Ligi Kuu Zanzibar kwa matokeo ya 0-0 dhidi ya Fufuni, kisha kuichapa Mwenge 2-1, hivyo imerejea Unguja ikiwa na pointi nne.