Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais wa Simba, MO aangalia fursa za uwekezaji Botswana

Muktasari:

  • MO, ambaye ni Rais na Mwekezaji wa Simba, amefanya mambo makubwa kwenye timu hiyo katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuisaidia kutwaa makombe kadhaa ya ndani, lakini pia kuiwezesha kuwa miongoni mwa timu tano bora barani Afrika kwa viwango vya soka.

GABORONE, BOTSWANA: RAIS wa Simba, Mohammed Dewji (MO), anaangalia fursa mpya za uwekezaji nchini Botswana baada ya kufanya mikutano ya ngazi ya juu iliyojikita katika mabadiliko ya uchumi wa nchi hiyo, mazingira ya uwekezaji na ukuaji wa sekta binafsi.

MO, ambaye ni Rais na Mwekezaji wa Simba, amefanya mambo makubwa kwenye timu hiyo katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuisaidia kutwaa makombe kadhaa ya ndani, lakini pia kuiwezesha kuwa miongoni mwa timu tano bora barani Afrika kwa viwango vya soka.

Katika ziara yake jijini Gaborone, Dewji alikutana na Rais wa nchi hiyo, Duma Boko; Makamu wa Rais, Ndaba Gaolathe; Gavana wa Benki Kuu ya Botswana, pamoja na viongozi wa Botswana Stock Exchange.

Mikutano hiyo imefanyika wakati Serikali ya Rais Boko ikiendeleza Botswana Economic Transformation Programme (BETP), mpango mkubwa wa kupanua vyanzo vya uchumi zaidi ya utegemezi wa jadi wa almasi, kuvutia uwekezaji mpya na kujenga maeneo mapya ya ukuaji.

Mazungumzo hayo yaligusa fursa za kuongeza ushiriki wa sekta binafsi, pamoja na maeneo ambayo kampuni yake, Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), ina nia ya kuyachunguza zaidi, yakiwemo nishati jadidifu na huduma za kifedha.

Akizungumza na Mwanaspoti, Dewji, ambaye kila msimu amekuwa akitoa kiasi cha fedha kusaidia usajili wa wachezaji kwenye kikosi cha Simba, alisema mikutano hiyo ilimpa picha nzuri zaidi ya mwelekeo wa uchumi wa Botswana na dhamira ya nchi hiyo kutumia uwekezaji kama kichocheo cha ukuaji.

“Botswana imejenga msingi imara. Kilichonivutia ni umakini ambao nchi inaweka katika hatua yake inayofuata ya ukuaji. Kuna msisitizo wa kuvutia uwekezaji, kujenga viwanda vinavyoweza kushindana na kuweka mazingira ambayo sekta binafsi inaweza kustawi,” alisema Dewji, ambaye hivi karibuni alishiriki katika Tamasha la Kilele cha Simba Day.

MeTL Group imejenga shughuli mbalimbali za biashara barani Afrika katika sekta za viwanda, kilimo, nishati, usafirishaji na maeneo mengine.

“MeTL tunapoendelea kukua Afrika, tunaangalia masoko ambayo tunaweza kupeleka mitaji, uzoefu na dhamira ya kujenga kwa muda mrefu. Tunaona fursa nzuri Botswana na tunatarajia kuendelea kuchunguza maeneo ambayo tunaweza kuwekeza na kujenga thamani pamoja,” aliongeza Mo Dewji.