Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia: Amani, usafi na utulivu ni muhimu kuelekea AFCON 2027

Muktasari:

  • Akizungumza na wananchi wa Arusha leo Novemba 19, 2026, Rais Samia amesema ujio wa wageni utakuwa fursa muhimu ya kiuchumi kwa wafanyabiashara, watoa huduma za utalii, wamiliki wa hoteli na wananchi kwa ujumla, hivyo amewataka kutumia fursa hiyo kujinufaisha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka wananchi wa Arusha kudumisha amani na utulivu pamoja na kuhakikisha usafi wa mji huo kuelekea mashindano ya AFCON 2027, yatakayovutia wageni kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania, Kenya na Uganda.

Akizungumza na wananchi wa Arusha leo Novemba 19, 2026, Rais Samia amesema ujio wa wageni utakuwa fursa muhimu ya kiuchumi kwa wafanyabiashara, watoa huduma za utalii, wamiliki wa hoteli na wananchi kwa ujumla, hivyo amewataka kutumia fursa hiyo kujinufaisha.

Aidha, ameitaka Serikali kuhakikisha miradi ya miundombinu na huduma muhimu inakamilishwa kwa wakati ili wageni watakapowasili wakute mazingira safi na huduma zinazostahili.

Kuhusu changamoto ya maji katika eneo la Arumeru, Rais Samia amewahakikishia wananchi kuwa Serikali itashughulikia tatizo hilo ili kuhakikisha wanapata huduma ya maji, akibainisha kuwa ametenga Shilingi 500 bilioni kwa ajili ya miradi ya maji mkoani Arusha.

Rais Samia yupo mkoani Arusha kuanzia Novemba 19 hadi 21, 2026, ambapo Novemba 20 anatarajiwa kufungua mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi utakaofanyika Chuo cha Polisi Moshi, huku Novemba 21 akitarajiwa kutunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Chuo cha Kijeshi Monduli.