Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pacome aanza mdogomdogo

PACOME Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo aliumia kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita 2025-2026 dhidi ya JKT Tanzania ambapo kutokana na jeraha hilo ataukosa msimu huu mzima wa ligi.

KIUNGO Pacome Zouzoua, amepiga hatua ya pili ya uponaji wake wa jeraha la kifundo cha mguu ambapo sasa ameacha kutembea kwa msaada wa magongo.

Kiungo huyo aliumia kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita 2025-2026 dhidi ya JKT Tanzania ambapo kutokana na jeraha hilo ataukosa msimu huu mzima wa ligi.

Baada ya awali kutoa chuma kilichowekwa kwenye jeraha hilo, sasa Pacome amefanikiwa kupiga hatua ya pili, akianza kutembea mwenyewe bila msaada wa magongo mawili aliyokuwa akiyatumia kabla kumsaidia kutembea vizuri.Awali kiungo huyo Septemba 10, 2026 alifika kwenye mezoezi ya timu hiyo akiwa anatembea na magongo hayo, akienda kuona mazoezi ya kikosi hicho kabla ya kucheza mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United.

PACO 01

Juzi kiungo huyo alifika tena kwenye mazoezi ya timu hiyo akiwa bila magongo hayo akitembea taratibu akichechemea kwa mbali lakini akionyesha kufurahishwa na hatua hiyo akicheka na kupongezwa na wenzake.

Kiungo huyo amesema hatua hiyo ni kubwa kwake ambapo amemshukuru Mungu kwa kuendelea kupiga hatua za kupona jeraha lake hilo.

“Hatua kubwa naendelea kuipiga, namshukuru Mungu naendelea vizuri, nimefurahi tena kugusa nyasi hizi za uwanja nikitembea kwa miguu yangu,” amesema Pacome huku akiwa na tabasamu usoni mwake.

PACO 02

Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya jopo la madaktari wa Yanga, zinasema kuwa bado kiungo huyo ataendelea kuwa nje ya uwanja kutokana na kutakiwa kuanza hatua ya pili ya matibabu yake ambayo inaweza kuwa nje ya nchi.

“Hatua anayopiga mpaka sasa ni kubwa anapona vizuri, kufika hapa pia ni kitu ambacho tunamshukuru Mungu lakini bado ana safari kidogo ya kuwa sawa, tunatarajia wakati wowote anaweza kuanza hatua nyingine ya kutafuta kupona zaidi ambayo inaweza kuanza nje ya nchi.”