Okwi akaribia Kaizer Chief
Wachezaji wa Massive FC wakijiandaa kwa pambano lao la fainali ya Kombe la Pamba Roho dhidi ya Dream Team litakalochezwa uwanja wa Bomani hapo kesho. PICHA NA HAMISI NGOWA
MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM INGAWA Simba inafanya siri kubwa lakini dili limevuja kwamba mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi, atafanyiwa vipimo kwenye klabu ya Kaizer Chief ya Afrika Kusini mwisho wa mwezi huu. Hiyo itakwenda sambamba na kusaini mkataba wa kazi baada ya kufuzu majaribio ya mwezi uliopita alipokwenda nchini humo. Habari zinadai kuwa benchi la ufundi la Kaizer limevutiwa na kiwango cha mchezaji huyo kuanzia Simba hadi kwenye timu ya Taifa ya Uganda. Ikiwa ataondoka, atakuwa mchezaji wa tatu kuiacha timu hiyo katika kipindi cha miezi miwili baada ya kuwauza wachezaji wake wawili, Mbwana Samatta na Patrick Ochan, ambao wamechukuliwa na TP Mazembe.