Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Pamba Jiji atuliza presha

PAMBA JIJI Pict

Muktasari:

  • Kibailo ambaye amekuwa na kiwango bora, hakusita kufichua kinachombeba akieleza kuwa kujituma na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ndio siri ya mafanikio yake akibainisha kuwa mpira ndio kazi yake.

PAMOJA na kukiri ugumu wa ligi, nyota wa Pamba Jiji, Hassan Kibailo amesema upepo mbaya walioanza nao ni sehemu ya matokeo ya mechi, akiahidi mapumziko waliyonayo watarejea wakiwa imara.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa hakuna tatizo lolote ndani au nje ya uwanja linalowafanya kutokuwa na matokeo mazuri, akiwatoa hofu mashabiki wasikate tamaa badala yake waendelee kuwasapoti.

“Hatuna tatizo lolote linalotuchanganya kwa matokeo haya, huu ni upepo mbaya umetuangukia na tunajua muda mwingine mpira unagoma, lakini hatujakata tamaa na tunaomba mashabiki waendelee kutusapoti.

PAMBA 01

“Kwa muda huu wa mapumziko tutajitathimini na kufanya masahihisho sehemu yenye tatizo na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi kuhakikisha tunaporejea uwanjani tunafanya vizuri,” amesema Kibailo.

Pamba Jiji haijawa na mwanzo mzuri baada ya kucheza mechi sita ikiambulia pointi moja, huku ikiwa imeruhusu mabao 13 na kufunga manne ikishika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

PAMBA 02

Kibailo ambaye amekuwa na kiwango bora, hakusita kufichua kinachombeba akieleza kuwa kujituma na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ndio siri ya mafanikio yake akibainisha kuwa mpira ndio kazi yake.