Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nne zaanza vibaya Ligi Daraja kwanza Unguja

UNGUJA Pict

Muktasari:

  • Kwenye msimamo wa kundi B, unaongozwa na Kundemba yenye pointi tisa sawa na ilizo Kitope United iliyopo nafasi ya pili inafuatiwa na Paje Star inayoshika ya tatu na pointi sita na New City iliyopo ya nne ikikusanya pointi tano.

LIGI Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja imeendelea huku timu nne zikishindwa kupata ushindi wowote tangu kuanza kwa ligi hiyo msimu wa 2026-2027.

Kati ya timu hizo, tatu ni za kundi A ikiwemo Bweleo Warriors, Kikungwi Stars na Malindi huku Rangers Bulls ikiwa timu pekee kutoka Kundi B ambayo haijapata ushindi wala pointi.

Msimamo wa kundi A wa ligi hiyo, unaongozwa na Taifa Jang'ombe yenye pointi 12 ikishinda mechi nne ilizocheza ikiwa haijapoteza mechi yoyote wala kutoa sare ndani ya ligi hiyo.

Nafasi ya pili ya msimamo huo inashikiliwa na New King iliyocheza mechi tatu ikishinda mbili na sare moja ikiwa na pointi saba ikiwa tofauti ya pointi tano na kinara wa kundi hilo, Negro United ikiwa nafasi ya tatu yenye pointi tano sawa na ilizonazo Mundu iliyopo ya nne.

Katika kundi hilo, Malindi iliyoshuka daraja msimu uliopita ipo nafasi ya mwisho ya msimamo wa kundi hilo lenye jumla ya timu tisa.

Kwenye msimamo wa kundi B, unaongozwa na Kundemba yenye pointi tisa sawa na ilizo Kitope United iliyopo nafasi ya pili inafuatiwa na Paje Star inayoshika ya tatu na pointi sita na New City iliyopo ya nne ikikusanya pointi tano.

Ranger Bulls ni timu pekee kwenye kundi hilo ambayo haijavuna alama hata moja baada ya kupoteza mechi tatu ilizocheza ndani ya ligi hiyo.