Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nkamia : Nitajenga umoja Simba, tusiwaze sana 20 Bilioni

Muktasari:

  • Kampeni za wagombea uenyekiti wa Simba zinazidi kusonga mbele kwa wagombea wawili waliopitishwa kuchuana kwenye uchaguzi mdogo utakaofanyika Februari 7 kuendelea kutambulisha sera zao na kujinasibu kwa wanachama wa klabu hiyo.


KAMPENI za wagombea uenyekiti wa Simba zinazidi kusonga mbele kwa wagombea wawili waliopitishwa kuchuana kwenye uchaguzi mdogo utakaofanyika Februari 7 kuendelea kutambulisha sera zao na kujinasibu kwa wanachama wa klabu hiyo.

Wagombea waliopenya kwenye mchujo na kuingia kwenye mbio za kutaka kumrithi Swedi Nkwabi aliyejiuzulu miezi kadhaa tangu alipochaguliwa,ni pamoja na katibu mwenezi wa zamani wa klabu hiyo, Juma Nkamia pamoja na Murtaza Mangungu.

Mwanaspoti limezungumza na Nkamia na kuweka bayana vitu gani vilivyomsukuma hata kuchukua fomu na kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi huo mdogo, msikieni mwenyewe anachokisema na jinsi alivyo na mipango kabambe kama atachaguliwa.

Kubwa analosema mbunge huyo wa zamani wa Chemba ni kutaka kuleta umoja ndani ya klabu. “Nataka kutengeneza umoja wa kutosha katika Simba,” anasema Nkamia aliyedai ndani ya Simba kuna watu wanaopinga mabadiliko, lakini akichaguliwa kuwa mwenyekiti moja ya mikakati yake ni kuwaelimisha maana ya mabadiliko na faida zake.

“Nilipokuwa msemaji wa Simba tulitwaa ubingwa wa Tanzania mara tatu, lakini wakati huohuo tumechukua ubingwa wa Kombe la Hedex mara mbili. Hata chachu ya mabadiliko ilianzia huko kwa sababu uendeshaji wa soka kwa wakati huo ilikuwa ngumu sana,” anasema Nkamia na kuongeza:

“Mimi na wenzangu wakati huo kina Kassim Dewji tuliona uendeshaji wa soka ni mgumu kidogo tukaanzisha kitu kinaitwa Friends of Simba.

“Friends of Simba ni kundi tuliloanzisha kwa lengo la kuisapoti Simba, ndipo tulipowaleta kina Mo Dewji kina Evans Aveva, Kaburu (Geofrey Nyange), wakaja kina Magori (Crescentius) wakaja kina Ngeleja (William). Ndipo tukapata watu wanaosapoti Simba na wamekuwa na mchango mkubwa kwenye Simba.”

Nkamia anasema kwamba hicho ndicho anajivunia kukifanya alipokuwa mwenezi wa Simba.

Kuhusu kampuni mbili za Simba Sports Club Consolidated na Simba Sports Club, Nkamia anasema kama atachaguliwa kuwa mwenyekiti hakutakuwa na migongano ya uongozi.

“Labda niseme kitu kimoja niliposikia Nkwabi amejiuzulu nilijiuliza maswali kwa nini amejiuzulu. Hajasema hadharani, lakini watu wake wa karibu wakawa wanasema inawezekana mwenyekiti wa Bodi ana nguvu zaidi kuliko mwenyekiti wa Simba upande wa wanachama.

“Sijajua ni nguvu za namna gani kwa sababu zingekuwa ni nguvu za kijeshi hilo ni suala lingine. Lakini kama ni nguvu za kukaa mkazungumza mkaelewana sidhani kama kuna tatizo kubwa. Mimi naamini Simba Sports Club Consolidated Company na Simba Sports Club Company Ltd ambayo iko chini Mo ambaye ndiye mwenyekiti wa Bodi kuna kuzungumza na kuna ‘memorandum of understanding’ kati ya pande hizi mbili,” anaongeza Nkamia na kuongeza:

“Kama pande hizi zilifikia hatua mpaka wakaanzisha hizi kampuni mbili sidhani kama kuna kitu kinaweza kushindikana.”

Simba Sports Club Consolidated ina jukumu la kusimamia hisa za wanachama na Simba Sports Club Company Ltd ina jukumu la kusimamia shughuli za kila siku za klabu.

Nkamia anasema katika kuweka mambo sawa watatafuta wataalamu wa kuwapa ushauri, wakiwamo wachumi na wanaofahamu masuala ya utawala. “Mimi sidhani kama kutakuwa na mgongano.”

“Ninachokiona hapo tatizo ni la cheo. Unajua wengi wanaamini cheo kionekane zaidi kuliko cha mwingine, kwa hiyo tutakwenda kufanya kazi kwa ajili ya kutengeneza mazingira mazuri ya klabu ya Simba na kwa uzoefu wangu naamini tutafika mahala pazuri,” anasema Nkamia.

Wachezaji na viongozi wa zamani Simba

Kuhusu utaratibu wa kuwaenzi wachezaji na viongozi wa zamani, Nkamia anasema akichaguliwa atahakikisha wachezaji na viongozi hao wa zamani wanaenziwa.

“Ni jambo lililokuwa likinisikitisha kidogo huwa nakutana na baadhi ya wachezaji wa zamani tunabadilishana mawazo, lazima ifike wakati tuwaenzi wachezaji wa zamani, pia nimepanga kama nitachaguliwa, nitaanza na hawa wachezaji wa zamani wako wengi wazuri kina Mogella (Zamoyoni), Mohammed Mwameja, kina George Masatu wako lazima tuwaenzi.”

“Lengo langu Simba isiwe Dar es Salaam. Nataka Simba iwe Tanzania nzima. Tunaweza kutengeneza kitu kinaitwa ‘road show’ tukafanya nchi nzima. Leo tukimchukua Zamoyoni Mogella au Mwameja tunaenda kufanya ‘road show’ ya kuhamasisha wanachama kule Ruvu, Chemba au kule kwenu Mwanza ama Shinyanga hiyo itakuwa njia ya kuwaenzi wachezaji wetu.”

“Nami naamini wako wangependa kumuona Zamoyoni Mogella waliosikia tu kuhusu nyota huyo wa zaani, pia wako waliosikia tu kuhusu George Masatu hawajawahi kumuona,” anasema Nkamia.

Pia, anasema lengo katika wilaya zote 186 za Tanzania wawe na matawi ya wanachama wa Simba, hiyo itafanikiwa tu kama wataweza kutengeneza kitu kinaitwa ‘road show’, kisha wachezaji wa zamani wakaenda nao huko. “Lakini na hao viongozi wetu angalau tuwe na utaratibu. Hilo tunaweza kulifanya hasa wakati wa ‘Simba Day’ badala ya kuwa michezo tu. Tukawa na jukumu la kuwaenzi wachezaji wetu wa zamani na viongozi wetu wa zamani ambao wamefanya kazi iliyotukuka.”

Hisa za Mo

Kuhusu hisa za Mo za Sh20 bilioni anasema wana Simba wasiwaze fedha kwanza. Hili tutakaa tutazungumza tutaangalia Mo kama aliji-commit atatoa hiyo pesa atatoa na kama ataitoa itafanyiwa nini. Ndio maana nasema pande zote zinazokubali mabadiliko na zinazopinga lazima wote tuwe kitu kimoja,” anasema Nkamia.