Nass kuzalisha kina Sakho, Mayele wapya
Kampuni inayojihusisha na ukuzaji wa michezo ya Nass Sports Solutions , imezindua rasmi mashindano ya “The After school Clash”.
Mashindano hayo ni kwa lengo la kuendeleza na kutia hamasa ya ushindani kwa wanafunzi waliomaliza ngazi zao za elimu ya kidato cha nne na cha sita katika ule mda wa likizo huku wakisubiria kuelekea hatua nyingine ya kimasomo.
Aidha Mkurugezi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Nassoro Mungaya amewakaribisha wadau mbalimbali kwa lengo la kumshika mkono ili kulifikisha jambo mbali.