Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nane zafuzu nusu fainali Dar Youth U-9, U-11

DAR pict

Muktasari:

  • Michuano hiyo ilianza majira ya saa 2:00 asubuhi na inatarajiwa kufikia tamati kesho baada ya kuchezwa kwa mechi za nusu fainali na fainali.

TIMU nane zimefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Dar Youth League kwa wavulana wenye umri chini ya miaka tisa (U-9) na miaka 11 (U-11) iliyoanza leo katika viwanja vya Ufundi, Lugalo, jijini Dar es Salaam, na kesho zitashuka dimbani kuwania nafasi ya kucheza fainali ya mashindano hayo.

Kwa upande wa U-9, Rising Youth SA itaumana na Magnet YSA, huku West FA ikiivaana na Aura Youth Tanzania katika michezo hiyo itakayobaini timu zitakazokutana kwenye fainali.

DA 01

Katika daraja la U-11, Aura Youth Tanzania itakipiga dhidi ya West FA, wakati Magnet YSA itachuana na Bulls FA kuwania tiketi ya kutinga fainali.

Timu hizo zimefuzu hatua hiyo baada ya kufanya vizuri katika hatua ya makundi ya mashindano hayo yaliyoanza rasmi leo, ambapo jumla ya mechi 36 zimechezwa.

DA 02

Kwa upande wa U-11, Aura Youth Tanzania ilimaliza kinara wa Kundi A kwa kukusanya pointi 12, ikifuatiwa na Bulls FA iliyopata pointi tisa. Katika Kundi B, Magnet YSA iliongoza kwa pointi tisa, huku West FA ikishika nafasi ya pili kwa pointi sita.

Kwa upande wa U-9, West FA ilimaliza kinara wa Kundi A kwa kukusanya pointi 12 baada ya kushinda mechi zote nne ilizocheza, huku Magnet YSA ikishika nafasi ya pili kwa pointi tisa baada ya kushinda mechi tatu na kupoteza moja.

DA 03

Katika Kundi B la U-9, Rising Youth SA ilimaliza kinara kwa pointi 12, huku Aura Youth Tanzania ikishika nafasi ya pili, na hivyo timu hizo kufuzu hatua hiyo ya nusu fainali.

Michuano hiyo ilianza majira ya saa 2:00 asubuhi na inatarajiwa kufikia tamati kesho baada ya kuchezwa kwa mechi za nusu fainali na fainali.