Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kapera ajipanga upya Songea United

KAPERA Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyeitumikia Polisi Tanzania msimu wa 2020-2021, alirejea ndani ya kikosi hicho msimu wa 2025-2026, baada ya kuachana na TMA FC ya jijini Arusha inayoshiriki Ligi ya Championship, ingawa, aliondoka kwa makubaliano ya pande mbili.

MSHAMBULIAJI wa Songea United, Ramadhan Kapera amesema kwa sasa anajitafuta upya katika kikosi hicho, baada ya kukaa nje ya uwanja bila ya kucheza kwa muda mrefu, tangu alipoachana na maafande wa Polisi Tanzania dirisha dogo la Januari 2026.

Nyota huyo aliyeitumikia Polisi Tanzania msimu wa 2020-2021, alirejea ndani ya kikosi hicho msimu wa 2025-2026, baada ya kuachana na TMA FC ya jijini Arusha inayoshiriki Ligi ya Championship, ingawa, aliondoka kwa makubaliano ya pande mbili.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kapera amesema licha ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu, ila alikuwa anaendelea na mazoezi yake binafsi ya kujiweka fiti kwa takribani miezi sita, jambo lililomsaidia kupata nafasi ya kujiunga na Songea United.

“Nashukuru kwa nafasi niliyoipata Songea United, kukaa nje kwa muda mrefu hakujaniharibia malengo yangu kwa sababu bado nilikuwa nafanya mazoezi binafsi kwa wakati wote, nimeanza taratibu ila huu ndio mwanzo mpya kwangu,” amesema Kapera.

Nyota huyo aliyewahi kuzichezea timu mbalimbali za Mbeya Kwanza, Geita Gold, KMC FC, Ihefu kwa sasa Singida Black Stars na TMA FC, amesema kadri anavyopata nafasi ya kucheza anarejesha hali ya kujiamini, jambo linalomuongezea morali zaidi.