Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi abadili mfumo, ataka mabao Bamako

YANGA leo inashuka na mfumo mpya wa hesabu za kuhakikisha kipa wao anakuwa katika ulinzi mkali, lakini hapohapo wakaongeza akili mpya ya kutaka mabao dhidi ya Real Bamako.
Yanga katika mazoezi yao ya juzi na jana huko jijini Bamako kazi kubwa ilikuwa ni kusuka safu yao ya ulinzi ambapo mabeki walipewa mbinu za kuhakikisha wanawakabili kwa ubora washambuliaji wa wapinzani wao.
Makocha wa Yanga, Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze walikuwa na msisitizo wa umakini kwa mabeki wao kuhakikisha wanaongeza utulivu wa akili katika kuzuia na hata mabeki hao hao kuanzisha mashambulizi.
Upande mwingine mabeki wao wa pembeni nao walikuwa na kazi nyingine ya kuhakikisha wanakwua na ubora wa kupandisha mashambulizi na kupiga krosi zinazofika kwa washambuliaji wao.
Eneo hilo mabeki Joyce Lomaliza na Djuma Shaban walikomaliwa kuwa na krosi zinazowafikia washambulaiji wao, lakini hapohapo mara baada ya kupoteza mipira walitakiwa kukimbia haraka kurudi kwenye nafasi zao tayari kwa kuimarisha ulinzi.
Wakati wa krosi hizo za Lomalisa na Djuma makocha hao walikuwa wanazuia zile pasi nyingi za katikati wakitaka kuwahi haraka lango la wapinzani huku washambuliaji Fiston Mayele, Kennedy Musonda na Clement Mzinze wakionyesha ubora wa kufunga kwa kutumia krosi hizo.

BOSI TFF AKUBALI MZIKI
Bosi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Vedastus Lufano ambaye ni mkuu wa msafara wa Yanga nchini Mali, ameangalia maisha ya timu hiyo hapo hotelini kisha mazoezini kisha akasema ana imani kubwa na matokeo yatakuwa mazuri.
Lufano ambaye ni bosi wa Chama cha soka jijini Mwanza mwenye nguvu kubwa ya ushawishi alisema kwa muda mrefu alikuwa hajaiona Yanga juu ya maisha ya wachezaji wake akisema umoja walionao wachezaji utaipa matokeo mazuri leo.
"Ni muda sijasafiri na Yanga lakini hivi sasa nimejua kwanini hii timu imekuwa inashinda sana, niko nao hapa hotelini huu ni mfano mzuri na bora wa timu inayoishi kama familia moja wana furaha sana,"alisema Lufano.
"Mazoezini nako wanahamasishana sana kuhakikisha wanapata matokeo, unaona wanakosoana kwa upendo na kushauriana na kuwasikiliza makocha wao hii inanipa imani kubwa mchezo wa kesho (leo) watapata matokeo mazuri."