Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwape awakaanga Tegete na Nsa Job

DAVIES Musonda Mwape

MWANDISHI WETU KOCHA wa Yanga, Kosta Papic amesema Nsa Job na Jerry Tegete wanatakiwa kufanya kazi kubwa ili wasipokwe namba na mshambuliaji mpya, Davies Mwape. Katika tukio jingine, Papic ametangaza rasmi kuwa Yanga imeachana rasmi na mshambuliaji wao wa Ghana, Kenneth Asamoah kutokana na matatizo ya usajili. Mwape, ambaye alikuwa anaichezea Konkola Blades ya Zambia amesajiliwa na Yanga katika usajili wa dirisha dogo pamoja na kiungo wa JKT Ruvu, Juma Seif wiki hii. Akizungumza na Mwanaspoti jana Ijumaa jijini Dar es Salaam, Papic alisema: "Siwezi kusema ni nani atakaa benchi, kwani ninapaswa kumuangalia Mwape anavyocheza, lakini Nsa na Tegete wanatakiwa kufanya mazoezi makali ili kupata namba uwanjani." Papic alisema kwa vyovyote itakavyokuwa wachezaji hao watatu: Mwape,Tegete na Nsa watatakiwa kufanya mazoezi makali na kujituma ili kupigania namba uwanjani. Nsa Job amecheza mechi zote 11 mzunguko wa kwanza, bila kufunga bao, huku Tegete akiwa amefunga mabao sita, lakini bado amekuwa akilalamikiwa kwa kukosa mabao mengi. Mwape ambaye amewahi kuzichezea klabu za Afrika Kusini za Orlando Pirates na Jomo Cosmos amefunga mabao manne katika mechi tisa alizochezea Konkola msimu huu. Yanga ilianza mazoezi yake jana Ijumaa jioni katika Uwanja wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika huku ikiwa na wachezaji wake wa Ghana watatu waliowasili asubuhi. Wachezaji waliowasili jana Ijumaa asubuhi ni Yaw Berko, Ernest Boakye na Issack Boakye. Papic alisema usajili wa Asamoah umeshindikana katika klabu hiyo na sasa suala hilo limefungwa rasmi.