Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania arejea, asubiri ofa

HUSNA Pict

Muktasari:

  • Mpaja aliyeitumikia She Cooperate msimu mmoja wa 2025/26 akitokea Rayon Sports ya Rwanda na alikuwa na kiwango bora alipofunga mabao 10.

KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa She Corporate FC ya Uganda, Husna Mpaja amerejea nchini baada ya mkataba wake na klabu hiyo ya Rwanda kumalizika, huku akisema yupo tayari kusikiliza ofa zilizopo mezani kwa ajili ya kuendelea na safari yake ya soka.

Mpaja aliyeitumikia She Cooperate msimu mmoja wa 2025/26 akitokea Rayon Sports ya Rwanda na alikuwa na kiwango bora alipofunga mabao 10.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mpaja amesema uamuzi wa kurejea nyumbani umetokana na kumalizika kwa mkataba wake nchini humo bila kuongezewa mwingine, hali iliyomfanya kuamua kurejea Tanzania akisubiri kujua hatma yake.

Kiungo huyo mshambuliaji amesema kwa sasa hana mkataba mpya, hivyo amerejea nchini akiwa tayari kupokea na kusikiliza ofa kutoka kwa klabu zitakazohitaji huduma yake.

Amesema pamoja na kuwa tayari kwa changamoto mpya, bado hajafanya uamuzi wa ofa alizopokea na atazichambua kwanza kabla ya kuamua timu atakayochezea.

“Nimerudi kupumzika kidogo na kufikiria ofa gani inaweza kunifaa lakini pia nitangaalia timu ambayo naweza kucheza ili nirejeshe utimamu wa mwili naamini nitafanya maamuzi sahihi,” amesema Mpaja.

Baadhi ya timu za Tanzania zinatajwa kupeleka ofa kwa kiungo huyo na moja kutoka Rwanda ambako alitumikia timu mbili tofauti.