Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msimu: Simba sc inanikuza kiwango

Muktasari:

  • Msimu alijiunga na Simba msimu huu akitokea Coastal Union ya Tanga, iliyomlea tangu kikosi cha U-17 na U-20, kisha ikampandisha kucheza Ligi Kuu msimu wa 2024-2025 aliomaliza akiwa na mabao manne na 2025-2026 alikuwa na matatu, alisema kucheza kikosi cha Wanamsimbazi ni hatua kubwa kwake.

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bakari Selemani Msimu japokuwa haanzi moja kwa moja kikosi cha kwanza, lakini amesema hiyo siyo sababu ya kuacha kujifunza vitu muhimu vya kumjenga kuwa mchezaji mkubwa na tegemeo kwa baadaye.

Msimu alijiunga na Simba msimu huu akitokea Coastal Union ya Tanga, iliyomlea tangu kikosi cha U-17 na U-20, kisha ikampandisha kucheza Ligi Kuu msimu wa 2024-2025 aliomaliza akiwa na mabao manne na 2025-2026 alikuwa na matatu, alisema kucheza kikosi cha Wanamsimbazi ni hatua kubwa kwake.

“Nimejifunza vitu vingi, kubwa zaidi ni ufundi, mbinu na kufanya mazoezi ya ufiti, hivyo vimeongezeka kwangu na bado naendelea kujifunza ili kuwa mchezaji mkubwa wa kutegemewa kikosi cha kwanza kama ilivyo kwa wengine,” alisema Msimu na kuongeza;

“Simba ina wachezaji wageni na wazawa wenye levo za juu kwenye uchezaji, hivyo kuwa sehemu yao ni hatua kubwa kwangu ya kuendelea kuelewa napaswa kufanya nini ili niweze kufikia ndoto zangu.”

Msimu alisema msimu huu kwake ni wa tatu kucheza Ligi Kuu tangu alipopandishwa kikosi cha wakubwa 2024-2025 akiwa na Coastal na tangu ajiunge na Simba amecheza mechi tatu akianzia Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, kisha mbili za ligi dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold zote akiingia kipindi cha pili.

“Nafasi niliyopewa na kocha kucheza kwangu ina maana kubwa, ndiyo maana napaswa kuendelea kupambana kwani watu ninaocheza nao namba moja wana uzoefu na wana kiwango bora,” alisema Msimu.

Katika nafasi anayoicheza Msimu yupo Libasse Gueye ambaye msimu wa 2025-2026 alimaliza na mabao saba, huku msimu huu 2026-2027 anamiliki bao moja na asisti tano. Mwingine Elie Mpanzu msimu uliopita alikuwa na mabao saba na asisti 10, katika ligi ya msimu huu anamiliki bao moja.