Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mrwanda apata matumaini mapya Dodoma Jiji

DODOMA Pict

Muktasari:

  • Mashami aliyekabidhiwa kikosi hicho baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Amani Josiah kujiungana na maafande wa Mashujaa FC, alianza kwa kusuasua katika mechi tatu za mwanzoni za Ligi Kuu Bara, japo kwa sasa mwenendo wake ni mzuri.

BAADA ya kushinda mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Mrwanda Vincent Mashami amesema kwa sasa timu hiyo iko katika mwelekeo mzuri wa kimuunganiko wa kiuchezaji, licha ya ushindani mkubwa unaoendelea msimu huu.

Mashami aliyekabidhiwa kikosi hicho baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Amani Josiah kujiungana na maafande wa Mashujaa FC, alianza kwa kusuasua katika mechi tatu za mwanzoni za Ligi Kuu Bara, japo kwa sasa mwenendo wake ni mzuri.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mashami amesema mechi tatu za mwanzoni zilikuwa ni ngumu zaidi kwake kutokana na baadhi ya wachezaji kutokuwa na muunganiko mzuri wa kiuchezaji, huku presha ya kutofanya vizuri ikichangia pia kwa kiasi kikubwa.

DODO 01

“Ni kazi kubwa sana wakati unatengeneza muunganiko wa timu kiuchezaji ila wakati huo huo mwenendo sio mzuri, tunashukuru baada ya mechi zetu tatu zilizopita zimetuongezea mwanga na morali ya wachezaji kufanya vizuri zaidi,” amesema Mashami.

Mashami amesema katika kipindi hiki cha kupisha kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), hawatokuwa na mapumziko marefu kwa wachezaji, isipokuwa wametoa wiki moja na kurejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo.

“Tunahitaji kutumia kipindi hiki cha mapumziko kufanyia kazi changamoto zilizopo kikosini, hasa kutengeneza muunganiko mzuri wa kiuchezaji na kuleta balansi katika maeneo mawili ya kujilinda na ushambuliaji,” amesema.

DODO 02

Katika mechi sita za Dodoma Jiji msimu huu Ligi Kuu Bara, Mashami alianza kwa sare ya bao 1-1, dhidi ya Pamba Jiji, Agosti 14, 2026) na kupoteza mbele ya Mbeya City 2-0, Agosti 19, 2026, kisha (1-0) v Polisi Tanzania, Agosti 25, 2026.

Baada ya hapo, kocha huyo alishinda mechi tatu mfululizo na kurejesha matumaini ya kikosi akianza kwa kuichapa TRA United bao 1-0, Agosti 29, 2026, (1-0) v Mashujaa FC, Septemba 4, 2026, kisha (1-0) v Namungo FC, Septemba 11, 2026.