Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco awakalia kooni mastraika TRA United

MOROCCO Pict

Muktasari:

  • Morocco ametoa kauli hiyo baada ya TRA United kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Novemba 22, 2026, Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

KOCHA wa TRA United, Hemed Suleiman ‘Morocco’, amewataka washambuliaji wake kuongeza utulivu wanapofika eneo la mwisho la wapinzani ili waweze kutumia vizuri nafasi za kufunga, akisema tatizo hilo limekuwa likiinyima timu yake ushindi licha ya kutengeneza nafasi nyingi.

Morocco ametoa kauli hiyo baada ya TRA United kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Novemba 22, 2026, Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Kocha huyo amesema timu yake ilikuwa na uwezo wa kuondoka na pointi zote tatu, lakini kushindwa kutumia nafasi za wazi ilizozitengeneza kuliigharimu na kuifanya ipoteze pointi mbili muhimu.

“Baadhi ya washambuliaji wetu bado wanakosa utulivu wanapokuwa kwenye nafasi za kufunga. Hili ni tatizo ambalo linatupunguzia kasi ya kupata ushindi kwa sababu tunakuwa tumefanya kazi kubwa ya kutengeneza nafasi, lakini tunashindwa kuzimalizia,” amesema Morocco.

MORO 01

Ameongeza benchi la ufundi linaendelea kulifanyia kazi tatizo hilo ili kuhakikisha wachezaji wanakuwa na utulivu zaidi wanapofika mbele ya lango la wapinzani na kubadilisha nafasi wanazopata kuwa mabao.

“Tunaendelea kulifanyia kazi tatizo hilo. Tunahitaji wachezaji wetu wawe na utulivu zaidi wanapokuwa mbele ya lango ili tuweze kubadilisha nafasi tunazopata kuwa mabao na kupata matokeo tunayoyahitaji,” amesema.

Akizungumzia matokeo dhidi ya Kagera Sugar, amesema sare hiyo hawakuitarajia na kiwango cha timu yake kilikuwa kinawapa nafasi ya kuondoka na ushindi.

“Tulistahili kupata ushindi kwenye mchezo huu, lakini tumeshindwa kujitengenezea matokeo tuliyokuwa tunayataka. Tulipata nafasi ambazo kama tungezitumia vizuri, tungeweza kuondoka na pointi tatu,” amesema.

Katika mchezo huo, Kagera Sugar ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao kupitia Yassin Saleh dakika ya 43, kabla ya Amy Mapaka kuisawazishia TRA United dakika ya 57 na kufanya timu hizo zigawane pointi.

MORO 02

Sare hiyo imeifanya TRA United kufikisha pointi 12 baada ya kucheza mechi 11, ikiwa imeshinda mbili, sare sita na kupoteza tatu, matokeo yanayoifanya kukaa nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

TRA pia imefunga mabao 11 na kuruhusu idadi hiyo hiyo, hali inayodhihirisha kuwa pamoja na changamoto ya ushambuliaji, timu hiyo inahitaji kuboresha matumizi ya nafasi inazotengeneza ili kuongeza idadi ya ushindi.

Ushindi wa TRA United msimu huu ni dhidi ya Pamba Jiji iliyoichapa mabao 3-1 na Fountain Gate iliyoifunga 3-2. Sare ilipata dhidi ya JKT Tanzania (1-1), Coastal Union (1-1), Mbeya City (0-0), Yanga (0-0), Geita Gold (1-1) na Kagera Sugar (1-1).

Baada ya matokeo hayo, TRA United sasa inajiandaa kwa mechi ijao dhidi ya Mashujaa itakayochezwa ugenini Novemba 28, 2026 kabla ya kuikaribisha Polisi Tanzania Desemba 4, 2026 na Simba Desemba 11, 2026.