Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA United yachekelea maandalizi Ligi Kuu

TRA Pict

Muktasari:

  • TRA United ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 11 baada ya mechi 10, wakati Kagera Sugar ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi sita baada ya mechi 11. TRA ilikuwa imefunga mabao 10 na kuruhusu 10, huku Kagera ikifunga tisa na kuruhusu 22.

TRA United inaelekea Bukoba kukutana na Kagera Sugar Jumapili, Novemba 22, 2026 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Kaitaba, ikiwa na dhamira ya kuendeleza ushindani wake na kurejea na pointi tatu.

TRA United ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 11 baada ya mechi 10, wakati Kagera Sugar ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi sita baada ya mechi 11. TRA ilikuwa imefunga mabao 10 na kuruhusu 10, huku Kagera ikifunga tisa na kuruhusu 22.

Kocha wa timu hiyo, Hemed Suleiman ‘Morocco’ anaingia kwenye mchezo huo akiwa na nafasi ya kutumia mapumziko ya mechi za kimataifa kuimarisha kikosi chake ambacho hakikuanza vizuri, huku akitaka kuona maboresho yaliyofanyika yakizaa matunda dhidi ya Kagera Sugar.

TR 01

Mchezo huo unakuja wakati Kagera ikiwa na uhitaji wa kuboresha matokeo yake, huku TRA nayo ikitaka kuendeleza mwenendo wake baada ya kuanza msimu ikiwa na changamoto ya kupata ushindi.

Kocha huyo amesema mapumziko ya wiki za kimataifa yamekuwa na manufaa kwao kwa sababu yamewapa nafasi ya kufanya tathmini ya changamoto zilizokuwa ndani ya kikosi na kuzifanyia kazi kabla ya kurejea kwenye ligi.

“Mapumziko haya yametusaidia sana kwa sababu tumepata muda wa kuangalia changamoto tulizokuwa nazo ndani ya kikosi na kuzifanyia kazi. Tumekuwa na nafasi ya kuboresha maeneo mbalimbali ili kurejea tukiwa imara zaidi,” amesema Morocco.

Akizungumzia mchezo dhidi ya Kagera Sugar, amesema wanakwenda Bukoba wakiwa na hesabu za kutafuta ushindi, akisisitiza umuhimu wa kupata matokeo mazuri katika mchezo huo.

TR 02

“Tunajua tunakwenda kucheza na Kagera Sugar katika uwanja wao, lakini maandalizi yetu yamelenga kupata ushindi. Tunaiheshimu timu hiyo, lakini tuna malengo yetu na tunataka kuyafanikisha,” amesema.

Morocco pia aliushukuru uongozi wa TRA United kwa kuwasafirisha kwa ndege kwenda Bukoba, akisema hatua hiyo itasaidia kupunguza uchovu kwa wachezaji na kuwapa nafasi nzuri ya kujiandaa kwa mchezo huo.

“Niwapongeze viongozi wetu kwa kutuwezesha kusafiri kwa ndege. Hii itatusaidia kupunguza uchovu wa safari na kuwapa wachezaji muda mzuri wa kupumzika na kujiandaa kwa mchezo,” amesema.

Mchezo huo utapigwa Jumapili, Novemba 22, saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, ukiwa unasubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na matokeo ya timu zote.