Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mlandege yafanya mabadiliko ya uongozi

MLANDEGE Pict
MLANDEGE Pict

Muktasari:

  • Uongozi wa Mlandege umewaomba mashabiki, wanachama na wadau wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi na bechi la ufundi

UONGOZI wa klabu ya Mlandege umefanya mabadiliko madogo katika bechi la ufundi la timu hiyo pamoja na Kitengo cha Habari na Mawasiliano.

Katika mabadiliko ya bechi hilo la Ufundi, Said Omar Kwimbu ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu, kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Bechi la Ufundi la Mlandege.

Naye, Hassan Ramadhan ‘Pele’ aliyekuwa Kocha Mkuu, ameteuliwa kuwa Kocha Msaidizi, huku Sabri Ramadhan China atakuwa Kocha wa viungo, awali alikuwa Kocha Msaidizi.

Pia, uongozi wa Mlandege umesitisha mkataba wa utumishi na aliyekuwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Hemed Abdulraman baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Aidha uongozi wa timu hiyo umemteua Ibrahim Adam Nyakunga kuwa Kaimu Ofisa Habari wa timu hiyo huku mchakato wa kutafuta Ofisa Habari mwingine ukiendelea.

Uongozi wa Mlandege umewaomba mashabiki, wanachama na wadau wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi na bechi la ufundi