Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKU yautaka ubingwa Ligi Kuu Zanzibar

JKU Pict

Muktasari:

  • JKU itashuka dimbani Novemba Mosi, 2026 kucheza dhidi ya Fufuni kwenye Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.

KOCHA Mkuu wa JKU, AbdulSaleh Mohammed, ametangaza mikakati ya kuisuka upya timu hiyo ili kuhakikisha wananyakua ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) huku akisisitiza kuwa nafasi ya pili wanayoshikilia ni chachu ya kuongeza juhudi na si sababu ya kukata tamaa.

Akitangaza mipango hiyo wakati akizungumza na Mwanaspoti, kocha huyo alieleza kuwa ingawa wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, mbio za ubingwa bado zipo wazi na benchi la ufundi linashughulikia makosa yaliyojitokeza katika michezo iliyopita.

“Nafasi ya pili inatupa picha ya kurekebisha makosa na kuandaa mipango mizuri kwani Ligi bado ni ndefu na ushindani ni mkubwa, lakini lengo halijabadilika tunataka ubingwa.”

Kocha huyo ameongeza kuwa, eneo kubwa analolifanyia kazi kwa sasa ni safu ya usambuliaji ili kuongeza umakini wa kufunga mabao, pamoja na kuimarisha nidhamu ya ulinzi wakati timu inapocheza chini ya shinikizo.  Mbali na hayo, aliwapongeza mashabiki wa JKU kwa kuendelea kuipa timu hiyo ushirikiano, na kuwataka wajitokeze kwa wingi katika michezo inayofuata ili kuwapa wachezaji hamasa.

JKU, ambayo ni miongoni mwa klabu kongwe na zenye historia kubwa katika soka la Zanzibar, inaendelea kukimbizana kwa karibu ikiwa pointi 18 na vinara wa ligi Zimamoto yenye pointi 19.

JKU itashuka dimbani Novemba Mosi, 2026 kucheza dhidi ya Fufuni kwenye Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.